Biashara ya juice ya miwa

kijazi07

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2016
Posts
1,031
Reaction score
2,186
Naomba kwenda moja kwa moja kwenye mada nataka kuanza hii biashara naomba mniambie upatikanaji wa mashine ya kukamulia miwa, soko la miwa linapatikana wap hapa dar es salaam pia changamoto ya hii biashara ni ipi ,,, pia kama una input yoyote naomba unishirikishe
 
Soko la miwa Tandika na Tandale Mashine kuna za kichina hapo kariakoo pia kuna zile za sido nenda sido utapata uliza lingine...
 
Nimewahi fanya hii biashara kikubwa huwe msafi ...vaa groves unapo kamua juice.....mashine zinauzwa kuanzia laki 8 na kuendelea ila kwa apo dar sijajua zipo wapi
 
Biashara ya miwa
Mashine milion 1.8
Miwa bando moja ni 11000 ambayo inaleta jumla ya shilingi elfu 34 faida (23,000)
Tangawizi za buku 2
Pesheni za buku
Barafu unanunua za elfu 10 kwa bando 7 za miwa
Glass 15
Jagi 2
Mirija elf 6
Sahani kubwa ya bati elfu 3
Umeme na kibanda/meza
Ndoo mbili au 3 na chujio

Wafanya kazi 2
1.Mkamuaji
2.Muuzaji
 
Bando moja linauzwa elfu 11 linakuwa na miwa ya kutoa juisi glass 65 mpaka 75 za 500. Na barafu za elfu 5 zinawez kutumika kusukuma mizigo ya miwa 4. Hauna haja ya kununua sukari
Sasa kulikuwa na haja gn ya kuweka sukari hapo πŸ˜‚ kwamba ugeni wa biashara anaweza kuweka sukari kwenye juisi ya miwa πŸ˜‚
 
Usafi
Myuwa haisafishwi vilivyo, mabwana afya hawakagui mazingira inakotengenezwa matokeo yake magonjwa ya typhoid yanakuwa mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…