Biashara ya kahawa na kashata

magogu

New Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
2
Reaction score
1
Za jioni ndugu jamaa na marafiki.

Naomben msaada wenu wakina.

Nina mtaji wa 250,000/= nataka kufanya biashara ya kahawa na nipo Dar es salaam. Kabla sijaanza ningependa kuuliza maswali yafwatayo÷

UPANDE WA MUUZAJI
1/Mauzo kwa siku ni bei gani (kahawa na kashata) na hesabu kwa tajir bei gani?
2/je malazi ya muuzaji ni juu ya bosi au anajitegemea?

UPANDE WA TAJIRI/MWENYE BIASHARA
1/gharama ya vyombo (sinia la kashata, birika, vikombe) na vinapatikana wapi?
2/gharama za kahawa, kashata, mkaa na tangawizi kwa siku ni kiasi gani?
3/je kama malazi ya wafanyakazi wake ni juu ya tajiri. Je gharama za chakula? Na matibabu?
4/ili biashara iwe na faida na ilipe inahitaj vijana wangapi wa kufanya kazi?
5/changamoto zikoje kwa upande wa
A)usimamizi?
B)mfanyakazi kutoroka na vitendea kazi?
C)mfanyakazi hajaleta hesabu?
 
Kazi ipo hapa ngoja wenyewe waje vuta subira
 
Kati ya biashara ninazozionaga ngumu hiyo inaongoza..kikombe cha kahawa100 na kashata 100.. huyu kwa siku si anauza buku mbili tu huyu?..haf anatembea mji mzima kusaka mia!!!hapa utakua unaletewa faida ya buku kwa siku..hela ndogo sana hiyo haf eti apange chumba!!..mi huwa naona bora uuze madafu tu au mahindi ya kuchoma maana dafu/hindi unaweza pata kwa 300 ukauza buku mpaka 1500 hapo gharama ni baiskeli tu..
 
Nilichogundua hapa dar biashara zenye kudhaulika ndio zenye pesa Sana.

Ni kweli..kuna jamaa anauza kuku wa kukaanga kituo cha daladala, anauza zaidi ya kuku 20 kwa siku..kuku mmoja anamnunua elf 5 kisha yeye kwa kila kuku anapata faida ya zaidi ya buku 5..hii inamaanisha kwa siku anaingiza laki nne huku laki mbili ni faida..huyu halipi kodi yoyote halipi umeme, maji nk. na usafiri wake wa kubeba vifaa ni mkokoteni tu ambao hauna gharama..mtu huyu ana make kumzidi mtu mwenye restaurant anayelipa umeme maji wafanyakazi nk..kwa wiki anaingiza milioni ambayo haikatwi kodi..
 
Biashara usiyoijua wala usiisemee, kuna mtu alishawahi kunishangaza kwa biashara ya barafu tu!
 
Nilichogundua hapa dar biashara zenye kudhaulika ndio zenye pesa Sana.
Ni kweli mkuu kama ndoo ndogo ya karoti unanunua kwa buku tano buguruni alafu wewe unuziwa karoti mia mbili kuna faida kiasi gani? au wauza mahindi ya uchoma,nimewahi sikia stori ya mtengeneza kucha kuwa kwa siku amekosasana analaza elfu hamsini,kifupi mtu mchakalikaji ana posibilityya kutoka kimaisha kuliko mtu smart,yaani educated
 
Nilichogundua hapa dar biashara zenye kudhaulika ndio zenye pesa Sana.
Umesema kweli mkuu

Wabeba taka wanapesa sana...kila nyumba 1000 mtaa mmoja una nyumba zaidi ya 60..kwa siku anazunguka mitaa zaidi ya 10

Gharama yake ni msosi na mkokoteni..na pa kwenda kutupa....

Endeleeni tu kung'ang'ania kuvaa suti kwenye viyoyozi...
 
Sasa Si Mfanye Maneno Mengi Ya Nini ?? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hao jamaa faida wanapatia kwenye kahawa. Kashata wanagharamika sukari, karanga au ufuta, kuziandaa.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] we jamaa ni mkorofi sana.

Ooooh inalipa inalipa sawa FANYA !!

Hamna mkuu unajua kuna raia wanadhani kuyajenga ize ize tu. Ingia field fanya. Eeeeh ujue hela watu tunaitafuta ila sio rahisi as people think.

Hela ina codes mazee sio slope tu.
 
Una uhakika na hiki ulicho andika mkuu!?
 
Biashara ya kahawa na kashata serious mkuu

We have to think thing over .yaani inatupasa kufikiri Sana

Siku moja kak angu alinitoa mbeya na kunifungulia biashara ya kitimoto yaani mwanzo nilidhani kuwa Broo Ananisalilisha badal tutungue hadwaer yey anakuja nifungulia mnadukua ya kuuza kitimoto yaani sikuamini ndani ya mwezi moja faid nilifuka milion moja na nusu kwa mwezi tu sikuweza kuamini biahsra ilikuwa imekaa POA sana ile Ila baad ya mwez wa 12 biashta ilidorora sna had Kuja kufunga kwa kuona kuwa Kodi Ni kubwa ya pango na mauzo Ni madogo
 
Kuna dogo mmja kwa siku alikuwa abafunga mpk 20000
Ila kwa sasa 12000,10000 maana wauzaji wameongezeka
Kikubwa upate kijiwe kizuri

Ova
 
Una uhakika na hiki ulicho andika mkuu!?

Yeah..ile biashara haihitaji aibu, kijiwe chake kilikuwa kituo cha basi ila sasa kimeondolewa baada ya ujenzi wa mwendo kasi....

Mbona kawaida sana hiyo.. kuna mhindi kule town ameajiri watu wanauza mihogo ya kukaanga pale chini ya apartment yake . Kila kipande 500 na foleni yake balaa. yeye amewaroga watu kwa chachandu tu basi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…