Habari
Naomba kufahamu anayeijua biashara ya kuchimba mawe ya gypsum. Kwa maeneo ya kilwa au makanya. Gharama Hadi kiwandani ni kiasi gani, na faida ni kiasi gani
Nawasilisha
Karibu ndgu brown.
Mimi nina kitalu cha kuchimba gypsum stone na gypsum powder maeneo ya Bendera Mkomazi njia baada ya Bwiko ukiwa unatoka Dar.
Tunatoa gypsum stone na powder ambayo ni sulphate ake ni almost 80%
Gharama za kusafirisha mzigo toka hapo kwenye kitalu ni almost 1,150,000 hadi 1,200,000 kwa gari ya tonne 30 kupeleka hadi viwanda vya gypsum au vya cement vya dar maeneo ya mbagala kwa mbele nadhani ni kivule kule kwenye viwanda vya Dangote na Camel. Mara nyingi tumekuwa tukiwauzia wafanyabiashara na huleleka Dar, kitalu kimesajiliwa na kuna kijiko maalumu kwa ajili ya kuchimba na kukusanya mzigo.
Nakushauri kama unataka magari ya uhakika kukusafirishia mzigo na kwa guaranteed katika biashara yako tumia magari za moshi au himo kwenye kampuni sio kudandia njiani, mfano KANAAN TRANSIT, na nyingine za moshi.. maana ni rahisi upatikanaji wake otherwise wawe booked ila wana magari mengi.
Kingine unaweza kutumia madalali ambao mara nyingi wapo hapo MAKANYA mzani au Kwa Bon wana uzoefu wa kujuana na madereva wengi wa malori, pia HEDARU kuna madalali unaweza watumia ila changamoto za madalali kazi zao ni za kubahatisha bahatisha anaweza akapewa kazi na dereva yuko boda ya namanga akasubirisha, dereva akifika arusha anakutana na kazi imeiva hawezi kuiacha pesa anabeba anakukatia vumbi.
Ni hayo tu kama unahitaji biashara ya Gypsum stone and gypsum powder tafadhari nipigie kwenye namba hii chap tuyajenge
+255 712 36 33 58.
Karibu sana mkuu, hata kwa ushauri zaidi maana tumebobea kwenye gypsum raw materials.
Amock
View attachment 2190703