Biashara ya kukodi Wachumba feki yashamiri Vietnam

Biashara ya kukodi Wachumba feki yashamiri Vietnam

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Biashara ya kukodisha Wachumba feki Nchini Vietnam imezidi kushamiri na kuendelea kukua siku hadi siku ambapo Vijana wamekuwa wakikodisha Wachumba hao na kwenda nao katika sherehe za familia ili kuziridhisha Familia zao zinazowapa presha na mfululizo wa yale maswali ya ‘Ndoa yako lini?’.

Imeelezwa kuwa shinikizo hilo la kijamii la kuanzisha Familia limewalazimu Vijana wengi Nchini Vietnam kukodisha Wapenzi wa muda mfupi (Wachumba feki) ili kuridhisha au kuwatuliza Wazazi wao ambapo kwa mujibu wa ripoti, presha hiyo imekuza Biashara hiyo mpya ambapo Vijana wanatafuta wenza wa muda kwa matukio maalum kama mikutano ya kifamilia na sherehe za mwaka mpya.

Minh Thu ambaye ni Msichana mwenye umri wa miaka 30 alikodi Mchumba wa muda wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa Lunar Nchini humo ili kuwaridhisha Wazazi wake waliokuwa wakimtaka awe na mwenza ambapo Mchumba huyo alijitokeza akiwa na ujuzi wa kupika na ustadi wa mazungumzo jambo lililowavutia sana Wazazi wake bila kujua kwamba amekodiwa.

Msichana mwingine aitwae Khanh Ngoc ambaye alikodisha kijana wa kiume mwenye mvuto ili kuondoa presha kutoka kwa Familia yake kuhusu ndoa, amekiri kuwa kitendo chake hicho kiliongeza maelewano kati yake na Wazazi wake japo ni Mchumba wa uongo.
 
Back
Top Bottom