Biashara ya kunenepesha ng'ombe kuuza

Moneyowner

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
1,423
Reaction score
1,252
Bandugu fursa nyingine hiyo mtaji mdogo tu kama m2 ivi, especially kwa wale wa mikoani, tafuta sehemu yako yenye marisho mazuri, nunua ng'ombe hata watano kwa lak 2 au 3 , walishe vizuri uza baada ya miezi 2 ivi wakinenepa vizuri hapo unaweza uza kwa lak 5 au 6 kwa kila ng'ombe.
kwa anaetaka kujikomboa na magu fursa hiyo hapo
Nawasilisha
 
***
wapi wanapatikana kwa laki 2,3?
 
mikoani tumekua herbivorous mkuu nyama haziuziki unaweza nenepesha ng'ombe ukaishia kuchinja pasaka kwa hasira
 
Soko liko wapi? na lina uhakika upi? Nataka nami niifanye
 
Msimu wa kuanza kilimo au ukame mkoa wa shinyanga na jirani zake
Ndugu,kama kuna ukame,naye mtoa post kasema unawachunga miezi miwili wananenepa! Loh! hii ikoje? Au majani yataota kwa vile unataka faida? Nahisi kuna mahali hujaeleza vizuri kuhusu kitu kinaitwa "Vyakula vya Ziada" hasa kipindi cha kiangazi.
 
wanunuzi ni wale wanaosafirisha ng'ombe kupeleka Dar,ukiwa na ng'ombe wenye afya nzuri ni rahisi sana kuuza
Asante. Wanakadiriaje bei ya ngombe,kwa kilo au kwa macho? Na utajuaje kuwa huyu akinenepa utauza kwa laki 5 ikiwa umemnunua laki 2 au 3?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…