Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Bhbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Posts
714
Reaction score
210

Ninaomba kujuzwa wanajf wenzangu, je ni nafaka aina gani zinaweza kuwa na soko zuri hapa mjini Dar? Na je ni mtaji kiasi gani naweza kuanzia nao? Natanguliza thanks.


WADAU WANAOHITAJI MIONGOZO KUHUSU BIASHARA HII
Ndugu zangu wanajamii,

Mimi nilikuwa nataka ushauri wa biashara ya duka la nafaka na mazao ya muhimu ambayo ni chakula kwa binadamu; yenye mzunguko mzuri kwa biashara.

IFAHAMU BIASHARA YA MAZAO YA CHAKULA

Haijalishi watu ni masikini kiasi gani, wala hali ya kiuchumi ni mbaya kiasi gani, lakini chakula na hasa hasa nafaka kitabakia kuwa hitaji la msingi kabisa la binadamu likifuatiwa na mavazi na malazi. Katika biashara zote, biashara ya kuuza mazao ya chakula kama vile mahindi, mchele, unga wa sembe na dona, maharage, sukari, unga wa ngano na mafuta ya kula ndiyo itakayokuwa ya mwisho kudorora.

Mazao ya vyakula, hususani yale ya nafaka kama mahindi, mpunga, ngano, mtama, mihogo, maharage na jamii zake, pamoja na ulezi vimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuongeza fursa za kiuchumi kutokana na sababu kubwa kwamba vyakula hivi ni muhimu kwa binadamu wote duniani bila ya kujali rangi, dini, kabila wala eneo analotoka mtu. Kuanzia Afrika, Asia, Ulaya, Australia, mpaka Marekani ya kusini na Kaskazini, hakuna mtu asiyetumia nafaka hizi.

Sekta hii hufanya kazi katika ngazi tofauti kwenye jamii, kuanzia, ngazi ya kaya ambao mara nyingi hawa ni wakulima wadogowadogo wanaozalisha mazao haya kwa kiasi kidogo tu kwa ajili ya chakula cha kujikimu na familia zao na mara chache kwa ajili ya kuuza kupata fedha kwa ajili ya kununulia mahitaji mengine madogomadogo ya familia. Kuna wakulima wakubwa au makampuni yanayolima mazao ya chakula kwa ajili ya biashara, makampuni ya ndani na wafanyabiashara wakubwa wanaonunua na kuuza mazao ya chakula ndani na nje ya nchi na makampuni makubwa mengine hujihusisha na biashara hii kwa namna moja au nyingine kwa ajili ya soko la Kimataifa.

Wapo wafanyabiashara wanaojihusisha na kununua nafaka kama mahindi na mpunga halafu huenda kukoboa au kusaga, biashara ya kukoboa na kusaga mahindi kwa mfano ni maarufu sana jijini Dar es salaam hasa maeneo ya Manzese na Tandika. Wafanyabiashara hao hasa kina mama wengi wamenufaika sana na biashara hii na huwapatia kipato na faida nyingi. Kuna wanaojihusisha na utengenezaji wa vifungashio tu pamoja na kuweka nembo na wapo wanaojihusisha na uuzaji peke yake. Hawa wanamiliki maduka ya kuuza unga, mchele na nafaka nyinginezo kama maharage nk.

Katika mgawanyo katika sekta ya biashara ya mazao ya biashara, utakuta ni mamilioni ya watu, karibu asilimia 90 ya watu wote katika nchi zinazoendelea kama Tanzania hujihusisha kwa namna moja au nyingine na biashara au ukuzaji wa mazao ya chakula. Lakini bado kuna tatizo moja, watu wengi wanalalamika sekta hii kutokuwa na tija ya kutosha, watu hao wengi watakuambia, kilimo bwana hakilipi, mazao ya chakula ni biashara kichaa haitabiriki, wengine watakuambia kilimo cha mazao kinahitaji mtaji kama biashara zingine hivyo hawana uwezo wa kupata mitaji nk.

Wakati watu hao hasahasa wale wanaoishi mijini wakilalamika na kutoa sababu hizo kibao, bado wapo na wanaendelea kuishi mijini huku wakilalamika kupanda kwa bei ya unga wa sembe na dona. Ukiwauliza wanadhani sababu ya chakula kuwa bei juu kiasi hicho ni nini, wanakujibu majibu wasiyokuwa na uhakika nayo kama vile, mvua haikunyesha ya kutosha, wakulima hawana pembejeo, serikali mpya imekuja na sera mpya ya kupandisha vyakula bei, watu wengi wamekimbilia mijini, shamba hakuna tena walimaji, ni mbinu ya madalali wa mazao kujipatia faida kubwa nk.

Ni kweli pamoja na kwamba ukame unaweza kuwa chanzo kikubwa cha kupanda kwa kasi kwa mazao ya chakula hasa mahindi na mazao yake kama unga wa dona, unga wa sembe na pumba za kulishia wanyama, lakini swali moja la kujiuliza ni kuwa, mbona mazao mengine kama mpunga hayakuathirika kiasi hicho? Ina maana huo ukame ulichagua mahindi na maharage peke yake? Labda unaweza ukasema ni kwa sababu watu wengi hapa Tanzania chakula chao kikubwa ni ugali.

Sababu zote hizo kwa mfano ingelikuwa ni nchi zilizoendelea sidhani kama zingelikuwa na nguvu kama hapa kwetu, usalama wetu wa chakula kwa ujumla haupo imara na hii haiwezi kuwa ni kutokana na sababu hizo zilizotajwa hapo juu, Watanzania kuna hatua tunatakiwa kuchukua ikiwa tutataka kuondokana na hali kama hii nyakati zijazo.

Kama Taifa lilivyoamua kuachana na kutegemea umeme wa maanguko ya maji kama wa mabwawa ya mtera, Kidatu na mengineyo baada ya majanga ya umeme kama yaliyosababisha Richmond, Dowans na skendo zingine kibao za uneme, katika suala la mazao ya chakula pia zinatakiwa zichukuliwe hatua na mikakati mbalimbali. Na hatua hizo si kuiachia tu serikali peke yake, ni suala linalotakiwa kuchukuliwa kwa uzito na wadau wote kwenye sekta wakiwemo wakulima, wafanyabiashara ya mazao ya kilimo, makampuni mbalimbali na mashirika makubwa.

Tatizo kubwa la nchi kama Tanzania hatutumii teknolojia kuhifadhi mazao, kwa mfano mahindi yakishavunwa yangeweza kuhifadhiwa vizuri na kisha kuja kuuzwa baadae wakati wa upungufu wa mahindi lakini hili hufanyika kwa kiasi kidogo sana tena na serikali, kwa upande wa wafanyabiashara siyo wengi wanaofanya hivyo husubiri kwenda kununua tu yaliyokwisha hifadhiwa.

Ikiwa kama utaamua kuwa serious na biashara ya nafaka kwa kutumia teknolojia zinazowezesha mazao kama mahindi kukaa kwa muda mrefu pasipo kuharibika, unaweza kutengeneza pesa nyingi sana katika kipindi cha muda mfupi tu.

Wakulima wadogo kwa upande wao wakisha vuna mahindi mengi wengine huyatumia bila mpango mzuri mfano kutengenezea pombe za kienyeji na kuyauza bei rahisi jambo linayoyafanya yaishe ndani ya kipindi kifupi. Utakachokifanya ni kuwekeza fedha zako kwenye ununuzi wa mahindi au na nafaka nyinginezo kama maharage kipindi cha mavuno kisha unayahifadhi kitaalamu kwa muda wa miezi kadhaa tu au mwaka halafu unaangalia vipindi vyenye upungufu wa mazao ndipo unauza.

Kilimo cha mahindi pia watu wamekuwa wakitegemea mvua zaidi, na zinapokuwa haba na mavuno nayo huwa haba. Tazama zao kama mpunga na ngano, mchele na ngano huzalishwa kwa wingi na makampuni makubwa tena kwa kiasi kikubwa kwa njia za umwagiliaji na ndiyo sababu hata unaweza ukaona mazao haya hayawezi kuathirika sana na ukosefu wa mvua kama ilivyokuwa kwa zao la mahindi.

Faida za kutumia makampuni makubwa kuwekeza katika biashara ya uzalishaji na uuzaji wa mazao ya chakula ni kwamba, huzalisha ajira wakati huo huo yakihakikisha usalama wa chakula unakuwepo. Makampuni makubwa yanakuwa na mitaji mikubwa hivyo kuwa na uwezo mkubwa pia katika uhifadhi na utunzaji wa mazao hayo kabla ya kuuzwa au kutumiwa katika shughuli za kuzalisha bidhaa nyingine. Yanakuwa pia na uwezo mkubwa wa usafirishaji wa mazao katika maeneo mbalimbali ya nchi yanakohitajika au nje ya nchi.

Ndiyo maana nasema bado fursa ni kubwa katika sekta hii tofauti na vile watu wengi mijini wanavyofikiri. Mwaka huu wafanyabiashara waliothubutu tu hata kuanzisha biashara ya kuchukua mazao kutoka mikoa inayozalisha nafaka kwa wingi kama vile, Mbeya, Ruvuma, Sumbawanga, Morogoro na Iringa wengi wao wanacheka, hawawezi kukuelewa ukiwaambia eti biashara zimedorora kwani katika maduka yao kila kukicha watu ni foleni, utasikia wakisema, “nipimie unga kilo 5”, “ nipimie mchele kilo 10”, wengine, “naomba mchele wa mbeya super”, maharage ni shilingi ngapi?”, sembe imepanda tena?” nk.

Tabia ya watu kupenda kula unga wa sembe nayo kwa kiasi fulani inachangia uhaba wa chakula hususani mahindi kwani kiasi kinachopotea kwenye pumba baada ya mahindi kukobolewa ni kikubwa, wanaofanya biashara ya kukoboa na kusaga mahindi wanafahamu sana ni kiasi gani cha pumba kinachopotea. Na kwa bahati mbaya zaidi ugali au unga wa mahindi yaliyokobolewa ni hatari kwa afya za walaji. Unaweza kuona unga wa sembe kuwa ni mzuri machoni au unapokula lakini kiafya ni majanga makubwa, ni chanzo kikubwa cha magojwa yasiyoambukiza kama kisukari, presha na hata unene kupita kiasi. Ingawa dona nayo wakati mwingine inaweza kuwa siyo nzuri sana endapo mahindi yatasagwa bila ya kuaosha vizuri, lakini kama yatasafishwa kikamilifu na kuondolewa yale yaliyoharibika ndicho chakula kizuri chenye afya.

Kuna kasumba nyingine ya watu kutokupenda kula baadhi ya vyakula kwa kuviona kama ni vyakula duni vinavyostahili kuliwa nyakati za njaa tu, vyakula kama vile ugali wa muhogo, ugali wa mtama, uwele na magimbi. Tumezoea kula ugali wa mahindi, wali, viazi, ndizi, mihogo ya kukaanga au ya kuchemsha, tambi na kande tu, wakati vyakula kama ugali wa mtama ni chakula kizuri sana chenye virutubishi vingi na nyuzinyuzi zinazosaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni.

Fursa nyingine kubwa kwa wanaopenda kuanzisha makampuni ya kudili na mazao ya chakula hasa nafaka ni kama hii ya kuhakikisha kwa mfano kampuni yako inakuja na mbinu na mikakati mipya ya kijasiriamali kama vile kusaga nafaka na kuzifungasha(pack) katika ubora wa hali ya juu, mandhari ya kuvutia mahali unapofanya shughuli hizo ukizingatia mtu ni afya. Kuwa na nembo(logo) yako mwenyewe iayokutambulisha kibiashara ni muhimu pa. Kwa ujumla hakikisha kampuni yako inakuwa tofauti na kampuni au biashara nyingine zinazojihusisha na biashara ya mazao ya chakula au nafaka.

Ukishakuwa na jina, (brand) yako nzuri unaweza ukauza bidhaa zako kama ni unga wa mahindi unga wa ulezi, unga wa mtama, mafuta ya kupikia, maziwa au chochote kile kinachohusiana na nafaka au chakula nchi nzima na hata nje ya nchi kama vile unavyowaona makampuni kama akina Azam, METL, Azania, Tanga Fresh na wengineo .

Chanzo: jifunzeujasiriamali.co.tz

MICHANGO YA WADAU
PIA, SOMA:

- Biashara ya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi: Jifunze Utaratibu wa Kufuata, Changamoto, Faida na Uzoefu wa Wengine

 
Bhbm,

Mkuu biashara ya nafaka inalipa. unaweza jikita na mazao kama maharagwe, kunde, njegere, mbaazi nk. mtaji unategemea na uhitaji, anza hata kidogo kwa gunia kama 3 kwa kila zao ila fanya utafiti wa soko ili utakapotaka kujitanua isikupe tabu.

Goodluck
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako mzuri, God bless you.
 
Bhbm,

Mkuu mimi c pingani na wewe but nataka kukushauri jambo moja,

- katika swala zima la biashara ya nafaka ni bora ukajikita katika ku ad value au kuongeza thamani ya hizo nafaka.

1. Ni bora ukawa na ofisi yako mjini na jaribu kuyaongezea thamani hayo mazo kama vile kugred na kupark kabisa. Hapo utakuwa umeongeza thamani na utauza kwa bei ya juu, na unaweza tafuta hata supermaket tano tu za kuwa sambazia.

2. Hili la kununua mchele kutoka mbeya na kuja kuuza dar kama ulivyo hakuna cha maana sana mtu nacho pata zaidi ya ujanja ujanja wa kuchanganya. Mtu anachukua mchele wa mbeya na kuchanganya na mchele wa morogoro
- hii biashara ya nafaka c kwa mba inalipa sana ila ni ujanja ujanja unao fanywa na wauzaji kwa kuchanganya changanya. Anaweza chukua gunia la maharage safi akachanganya na nusu gunia la maharage mabovu ndo business inaenda.

- ila hili la ujanja ujanja ni la muda sana na si endelevu.

So jitajidi upate hata mashine ya kupaki kwenye mifuko, mfano ukipata mashine moja inayo itwa heavy duty sealing machine ni nzuri sana unaweza ukawa na vibarua wako wa kugred na wewe ukawa unapaki na kuuzia watu wa supermarket.

Hiyo mashine niliyo kuambia ni ambayo ina silidi kama vile totopark zinavyo kuwa zimefungwa kwenye vile viroba.

Kuna kampuni moja ya Kenya ina tengeneza vifungashio vizuri sana unweza cheki huko.
 
Wadau naomba ujuzi weno kwenye hi biashara. Je, nikianza na shilingi milioni 5 itanitoa? Je kuna changamoto zipi nitarajie kukutana nazo.

Binafsi napenda sana kujiajiri.Robert Kayosaki anasema kwenye kitabu chake cha Poor Dady Rich Dady ya kwmba a highly paid slave is still a slave. WanaJF naomba kuwakilisha hoja.
 
Milioni tano yaweza kukutoa au yaweza kushindwa kulingana na maswali yafuatayo:

Mkuu nafaka zinatofautiana maana kuna, mpunga, mahindi, maharagwe, mtama, uwele, ngano, soya, etc, sasa ni nafaka zipi utahitaji kuzinunua?

Utaenda kununua kwa njia ya kukopesha wakati wa kulima ili upate mavuno baadae? Au utasubiri kipindi cha mavuno?

Jiulize ni sehemu zipi za Tz unategemea kwenda kununua?

Soko lako litakuwa wapi?

Ni wewe mwenyewe unategemea utaifanya hii kazi au utaajiri watu/agents?

Usafirishaji je, utakodi au unao binafsi?
 
Moja ya changamoto uwe tayari wakati wote kuuza kwa bei ya kupangwa na serikali kwani serikali inaiingiliaga bei za mazao hasahas vyakula ili kuwalinda walaji(wananchi) waweza wewe uwe umenunua kwa bei kubwa.

Ukaambiwa uza kwa bei ya kupangwa na serikali uwe makini sana kwa mazao yanayoweza haribika kabla ya kuwa sokoni nakutakia biashara njema.
 
Wapendwa wangu nataka kufanya biashara ya kununua mahindi toka Morogoro, Iringa au Njombe niyauze hapa Dar es salaam kwa magunia. Nmefanya research fupi yakuuliza kama naweza kuuza sokoni K/koo, lakini competition ni kubwa sana.

Pia sina watu katika hiyo Mikoa wakuniuzia hayo mahindi kwa bei nafuu. Tatizo lingine ni bei za usafirishaji kutoka hizo sehemu.

Naomba msaada wenu. Mungu awabariki sana
 
Fanya na utafiti kuhusu usafiri wa kutoka huko pia.
 
Mkuu katika Dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa sana ni Bora ukafanya kitu inaitwa AD VALUE. Hayo mahindi yaongezee thamani kabla ya kuyauza, make bila hivyo kwa kweli biashara inakuwa ngumu kwa sababu itabidi uwe unafanya Ujanja ujanja ili uweze kupata angalau cha juu na ujanja ujanja huo ni pamoja na kutumia vipimo fake wakati wa kununua.

Na some time kuchanganya mahindi mazuri na ambayo kidogo si mazuri, na huu ujanja huwa ni wa muda tu so kikubwa ni kuyaongezea thamani.
 

Sijakupata fresh mkuu wangu, naomba nielekeze vizuri.
 
Wapendwa wangu nisaidieni mwenye mchanganuo wa hiyo biashara. Asanteni
 
Wapendwa wangu nisaidieni mwenye mchanganuo wa hiyo biashara.asanteni
Utafiti bubu niliofanya ni kwamba, mahindi mazuri kwa sembe kwa soko la Dar ni yale yanayotoka Kiteto, Dom, Singida na Tanga. Sijui kwa nini wenye milling machines wengi wanayapenda zaidi ukilinganisha na ya nyanda za juu kusini.

Halafu siku hizi hata mikoani kuna milling machines pia, kwa hiyo utaona hoja ya kuongeza thamani bidhaa zako inapata mashiko zaidi kwa karne hii.
 

Kama hutojali unaweza kuniambia gunia moja kwa hizo sehemu ulizonitajia ni how much? Na kusafirisha hadi Dar kwa gunia ni sh ngap? Asante sana.
 
kama hutojali unaweza kuniambia gunia moja kwa hizo sehemu ulizonitajia ni how much? Na kusafirisha hadi dar kwa gunia ni sh ngap? Asante sana

Mkuu bei ya mahindi katika kipindi hiki mpaka march haiko stable, inapanda kila siku. Last week bei ya juu ilikuwa 90,000/ kwa gunia la kilo 100 mpaka kilo 120. Hii ni bei ya hapo Iringa, sijui week hii. Sijajua gharama za usafirishaji kama unakodi gari.
 
cjakupata fresh mkuu wangu, naomba nielekeze vizuri

Kuongeza thamani ni unayakoboa na kusaga kisha kupack kwenye mifuko ya mfano kg 25,10,5.then unayauza sehemu mbalimbali katika maduka,etc,au unafungua outlet mwenyewe na kuwa supplier kwa mawhosaler etc.
 
Mahindi ya Kiteto yanatoa unga mwingi kuliko mahindi ya nyanda za juu kusini kwa wastani mahindi ya Kiteto Dodoma yanatoa viroba 280 vya kg 25 na pumba 40-45 gunia wakati ya Iringa Songea yanatoa wastani wa viroba 260 kama una anza biashara ya mahindi kipindi hichi mahindi yapo juu sana kwakuwa yanapatikana kwa tabu sana.
 

Viroba 280 vya unga kwa mahindi ya uzito gani? kilo 100,200 au 100?
 

Mkuu wanasema mahindi Dodoma ni mazito sana na yana unga mwingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…