Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Wandugu poleni na mihangaiko ya kila siku hususani katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Moja kwa moja nije kwenye mada, mwaka jana nilijikita sana kwenye biashara ya zao la mpunga yaani nilikuwa nalima na kununua ila biashara inakua ngumu kidogo kulingana na bei inayokuwa sokoni kwa muda huo.

Mwaka huu nategemea kufanya biashara ya mahindi yani ninunue na kuyahifadhi kwenye magodauni ya watu na nije niyauze miezi ya masika pale bei zitakapopanda .

Hili ni wazo nililolipata kutoka kwa marafiki walionishauri niachane na kununua zao la mpunga nijikite kwenye mahindi kwani yanalipa sana kama utaweza yaweka mpaka pale bei zitakaposimama.

Sasa ningependa nisaidiwe ushauri hapa jukwaani kwa sababu najua hapa kuna wajuzi wa mambo kama haya.

Je, ni kweli hii biashara ya kuweka mahindi na ukayauza kipindi cha masika inaweza kulipa kweli a je, changamoto zake zikoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara ya mazao iko vizuri ukiwa na mtaji mkubwa, nunua sasa hivi bei ya chini uza mwezi wa kwanza au wa pili mwakani bei muda huo huwa iko juu sana.

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
 
Mkuu uko wapi kwa sasa biashara ya mazao inatakiwa uende na msimu ...kwa sasa ni msimu wa maharage ya ukanda wa mbulu kwa watu wa Arusha wanaelewa ..kununua na kuweka stoo ni kamari bei inaweza kushuka kuliko hata uliyonunulia pia inafanywa na watu wenye mitaji mikubwa

Wajanja wa mazao wanaenda na msimu pia unaweza ukaweka stoke ikakutana na msimu mwingine hapo tayari umeingia cha kike.kama uko pande za Arusha tembelea mbauda kupata maelekezo zaidi
 
mara nyingi watu wa mazao huwa wanafikiria kuweka stock alafu bei ikipanda ndo waanze kuuza.

mm nataka nianze mwezi ujao ila sifikirii kuweka stock.nataka ninunue niuze nifatate tena mzigo niuze. Nafaka ni nyingi kwa kuwa naanza sitoweza kufata mzigo mwenyewe ni mchele na maharage tu ndo nitafata mwenyewe nafaka zingine ntaletewa na wakulima kwa bei nafuu mpaka nilipo.

Nimejipanga kihivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa nipo Songea Ruvuma ,mtaji mkubwa kuanzia kiasi gani ndugu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu biashara ya mazao ina lipa kutokana na, the more you add value, the more you create the margin, mfano: Ukinunua mahindi then ww ukasaga na kuupaki na kuuza kama unga bei ni tofauti na aliyeuza mahindi
 
Mimi hi biashara inaniogopesha,hivi ukistock mahindi hayabanguliwi kweli,,ile dawa wanayoweka inakuaga effective 100%?
Ipo dawa moja ya kenya nimesahau jina lake, ila ni 180000 hiyo ndy effective, mdudu hapiti..unakuta mahind yako njema..

Saiv kinachosumbua ni kigezo cha moisture
 
Mimi hi biashara inaniogopesha,hivi ukistock mahindi hayabanguliwi kweli,,ile dawa wanayoweka inakuaga effective 100%?
Bwana biashara ya kuhifadhi mahindi ni pasua kichwa!!! Kutokana na ugumu wa ku ya hifadhi, na hilo ni kutokana na dawa nyingi kuwa fake!!! Unaweza kuja kukuta sio mahindi tena bali ni unga, asilimia kubwa serikali ndio huwa wanaweza kwani wao gharama ya kupulizia dawa sio inshu kwao na kupata dawa halisi.
 
Hapa kwenye dawa sio ishu maana wataalamu wapo watatuambia ,ila nasikia wanatumia vidonge vinavyowekwa kati ya gunia na gunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kwenye dawa sio ishu maana wataalamu wapo watatuambia ,ila nasikia wanatumia vidonge vinavyowekwa kati ya gunia na gunia

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, ila utunzaji wa mahindi gharani huwa ni shughuri ngumu sana, tena kwenye maghara haya ya watu binafsi ambao usafi kwao ni tabu, na kuna kuwa na mchanganyiki wa mazao, tofauti tofauti!!!
 
Ipo dawa moja ya kenya nimesahau jina lake, ila ni 180000 hiyo ndy effective, mdudu hapiti..unakuta mahind yako njema..

Saiv kinachosumbua ni kigezo cha moisture


Solution hapo nadhan bora usage upack! Jamani sozi wa morogoro ni milionea msukuma yule! Ana unga mzuri sana sana ..ameshika moro yooote! Had dona lake ni super...anaosha mahindi balaa ..! Sio machine zingin zinasaga tu dona linanuka pumba
 
Sawa, ila utunzaji wa mahindi gharani huwa ni shughuri ngumu sana, tena kwenye maghara haya ya watu binafsi ambao usafi kwao ni tabu, na kuna kuwa na mchanganyiki wa mazao, tofauti tofauti!!!
Atumie njia ipi mbadala sasa mkuu.
Naona umemuacha bila kumpa mbadala.
 
Mkuu unapanga kuwa na stock ya kuanzia gunia ngapi?

Kama utakuwa mzigo wa kawaida nunua na kuuuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…