Wadau kuna hili wazo la biashara ya kununua nguruwe huko Morogoro kuchinja na kuleta hapa Dar, ofcourse itahitaji uwe na order kwenye vituo vya kuuzia nyama ya nguruwe, kwenye mabaa na watu binafsi.
Unanunua nguruwe wa 100 kg kwa TZS 300,000/- unachinja na kuondoka na nyama fasta hadi Dar unaanza kusupply. Unaweza beba wawili hadi wanne kutokana na usafiri unaotumia na maandalizi uliyoweka.
Kama wapo wadai ambao wanaielewa hii biashara mazuri na mabaya mnijuze tafadhali.
Samahani wa wadau ambao hii ni haramu kwao.
Natanguliza shukrani.