ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,154
- 4,184
Habari wadau;
Kuna biashara nyingi ambazo mtu anaweza kufanya kwa kutumi kompyuta yake.Mojawapo ni biashara kuuza au kutengeneza website.
Nimesema kuuza au kutengeneza kwa sababu utaalamu wa kutengeneza websites unaweza kuwa changamoto kwa baadhi yetu kwa sababu kuna mambo mengi ambayo yanahitaji ujuzi wa kipekee.Hivyo basi kwa wale ambao hawana ujuzi wa kutengeneza wanaweza kuwa wauzaji tu wa huduma hizi.
Pamoja na yote biashara hii inamalzimu mteja kuwa na uelewa wa maswala fulani ya TEHAMA ambayo anaweza kujifunza mwenyewe au anaweza kutafuta watu,au vyuo vinavyotoa mafunzo hayo ambayo ni basic kwa muda mfupi.
Mafunzo haya yanweza kuhusiana na mambo yafuatayo:
Ukishafahamu hayo na kuelewa vizuri basi unaweza tafuta sehemu ya kununua webspace kwa ajili ya kuuza.Yako makampuni mengi sana ambayo yanauza huduma za webhosting,email hosting nakadhalika kwa ajili ya resellers yaani wauzaji wadogo wadogo.
Kulingana na hitaji wako unaweza kuwa unawanunulia wateja wako kisha unawapa wao kwa ajili ya kutengeneza wenyewe au unaweza ukanunu space kubwa kisha kuigawanya kwa jaili ya kuuza kwa bei ambayo unaona inafaa.Ziko options nyingi sana kutegemea na uhitaji wako na uhitaji wa mteja wako(Kufahamu kuhusu makampuni bora kabisa katika kuuza huduma hizi na jinsi ya kuwalipa nitafute PM )
Ukisha fanya uamuzi wa wapi utanunua ni vyema ukaanda bajeti ya mwaka kama TZS 500,000 kwa ajili ya internetet na kununua huduma kwa hao wauzaji,Baada ya hapo usishau kutafuta mtu atakeyekuuzia domain names,na hata watu ambao ni wataalam wa webdesign ili unapopata mteja unaweza kumfanyia complete package huku na wewe ukiendelea kujifunza
Faida ya hii biashara inategemea na aina ya wateja ila kwa wastani profit margin yake inaanzi 10% hadi 350% yaani unaweza kupata faida mara 3.5. ya mtaji wako ndani ya muda mfupi.
Karibuni tuendelee na mjadala

- Webserver Administration
- Websites resellers training
- Web Programming
- Website Management
- Webhosting Management