Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji


Mgawanyo wa makundi katika biashara ya microfinance (tiers) unazingatia uwezo Yaani mtaji na uendeshwaji wake

Tier 1 hili kundi linajumuisha deposit-taking institutions ambazo ni banks na microfinance banks.

Tier 2, kundi hili wanatoa mikopo tuu, hawaruhusiwi kuhifadhi pesa yoyote ya mteja kwa sababu yoyote (non deposits taking microfinance)

Tier 3, SACCOs

Tier 4, community financial groups

Kwa mtu anayeanza biashara akianzia tier 2 ni nzuri sio sababu ya mtaji mdogo (minimum capital) peke yake yake bali hata zile operational standards zinakua nafuu. Unapoingia moja kwa moja kwenye tier1 ujue organogram na office zako lazima viwe vya standard ya bank kadri ya muongozo wa regulator
 
Ahsante Sana kwa alieomba ushauri napia ahsante Sana kwa wote waliotoa michango yao mizuri. Kupitia muomba ushauri na washauri wenyewe, na Mimi nimepata ufahamu make hili linanihusu. Ahsante sana
 
Mi naona hapo unapoamua kufungua ofisi ya mikopo ingekuwa vizuri zaidi ukachagua kundi mfano kina mama, hili kundi kidogo Ni waaminifu lakini kina Baba mbona utalia kilio cha mbwa?😃😃
 
Kati yenu kuna waliofungiwa kwa sababu za kutukana na kutishia wateja wenu.
 
Kaka mi nahitaji micro-credit kuna chimbo moja nahitaji nikafungue ofisi nahisi nitapiga noti naomba pia na muongozo lakini pia ushauri nikisajiri kwa hili jina nitakuwa sahihi? SIZYA MICRO-CREDIT COMPANY LIMITED

ASANTE SANA
Kwanza jina huwezi chagua kwakuwa unapoenda brela wanaangalia kama jina lipo au limeshachukuliwa. Kama bile unavofungua email unaweza kuwa unataka iwe namna flani lkn ikawa ishatumika kwahiyo usipate unachotaka. Binafsi nilifanikiwa kufungua kwa wepesi sana lakini pia kuna watu wawili niliwapa njia Rahsi sana ya jamaa alienisaidia hatua za kibali cha BOT na leseni ya wizara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…