xfactor
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 1,511
- 1,289
Habari zenu great thinkers,natumaini ni wazima japo mwenzenu siku yangu imeingia nyongo kwa kiasi kikubwa
Naandika huu uzi Kwa masikitiko makubwa sana kwa kweli.Nikiwa nahisi kudharauliwa wakati huohuo nasikitika kwa jinsi ambavyo waafrika tulivyojijengea picha ya kuonekana wavivu.
Leo kuna muhindi mmoja kanifuata kwa nia ya kunipa taarifa ya biashara anayofanya ili nimsaidie kupata wateja,biashara yenyewe ndugu zangu ni ya kuuza dissertations za masters ya marketing au business administration (Mnivumilie kwa kuchanganya kiingereza maana tafsiri za kiswahili sina uhakika nazo).Huyu muhindi hafahamu mimi natoka nchi gani ila inaonekana ana uhakika kuwa nchi yoyote ya Afrika hii biashara yake inafanyika ndio maana akanifuata,pia inaonekana ameshafanya huko nyuma hii biashara.
Imeniuma sana kwakweli kwasababu hili swala nilishawahi lisikia Tanzania watu wa vyuo tofauti wakibadilishana dissertation wengine wakinunua kabisa.Sikuamini mpaka leo nilipokutana na huyu muuza dissertation.Kama elimu ya sekondari ni siasa na chuo napo wanafunzi ndio wanafanya haya tena mwanafunzi wa shahada ya pili basi kama nchi tunapoelekea ni pabaya sana.
Nini cha kufanya?
Na nyie wadau mtatoa maoni katika hili,ila mimi ushauri wangu ni kwamba ifike wakati vyuo vyetu Tanzania vianze kutumia teknolijia ipasavyo.Wenzetu wana software ya plagiarism ambayo inatafuta kwenye database ya vyuo vyote na kwenye google kuangalia kama hiyo dissertation au idea yake umeikopi
sehemu.
Embu tulijadili hili kwa kina maana linaogepesha sababu wanafunzi wengi wa shahada ya pili wapo maofisini,sasa kama ndio wanazipata shahada zao kwa minajili hii sidhani kama wata deliver ipasavyo
Maisha ni kama kioo,ukicheka na yenyewe yanacheka