elvis richard
Senior Member
- Dec 6, 2014
- 195
- 207
Magari ya hapa Tanzania...yaliyotumiwa na wabongo achana na yale ya nje.Unataka kuuza magari yalotumika Tanzania au Japan? Tuanzie hapo kwanza
Ya hapa bongo aisee..unataa kuuza used ya kutoka nje ya tanzania au used za tanzania?? tuanzie hapo kwanzaa
Mimi niko mbeya...na kwa upande wa wateja ni wale wakutafutaUko mkoa gani? Wateja wako ni watu wanaokuzunguka au mpaka uwatafute?
Nilijaribu kuanza kupost magari nilikuwa nachukua picha Instagram pages za watu kisha napost WhatsApp status pamoja na fb lakini bado haikuleta tija sana.Uko mkoa gani? Wateja wako ni watu wanaokuzunguka au mpaka uwatafute?
Mhh ...nipo hapa hapa soweto na simfahamu huyo mtu ana yard ya magari??Kama upo Mbeya nenda maeneo ya Soweto ulizia kwa mtu Anaitwa SINANDUGU,atakusaidia pa kuanzia jamaa ni mtu mwema Sana.Biashara ya magari inahitaji ujenge uaminifu kwanza na ujuane na watu.
Hapo nduguyangu utachelewa. Kama hauna hobi ya magari basi wanaokuzunguka nao hawana hobby hiyo basi hauna network yakuuza magari. Labda uitengeneze, unaweza kuanza kwa kuanzisha biashara itayokuweka karibu na watu wa aina hiyo, mfano carwash, duka lakuuza oil au accessories za magari, sehem ya kuziba pancha nk. Then unaanza kulenga, mtu anashida anauza gari yake ukiiona nzuri unamlalia halafu unauza. Kama uko Dar jenga urafiki na madalali wa magari, huko utapata gari za bei nzuri na utapata wateja pia. Jiunge ba pages za wauza magari fb, nawewe unakuwa unapost huku unawinda za kulenga. Kikubwa kwanza ni kujenga hobby, hata hilo lako uza, hakikisha unabadili magari mara kwa mara, usiogope kuvunja gari kwa gari, gari kwa pesa na gari juu nkMimi niko mbeya...na kwa upande wa wateja ni wale wakutafuta
Kwa watu wanaonizunguka hawako interested sana na hivyo vitu
Anauza used spare parts,opposite na Mkulu HotelMhh ...nipo hapa hapa soweto na simfahamu huyo mtu ana yard ya magari??
Yaani mkuu uko hapo hapo Soweto na humjui sinandugu. hilo linawezekana kama hukuwahi kuwa na interest na magari, kwa Mbeya nadhani ndiye muuuzaji mkuu wa used spare parts za magari. Kiufupi nimeshuhudia yard za magari kama 2 hapo lakini biashara ni ya kusuasua sana. Hii yako ya kuuza magari used ya hapa hapa bongo yaweza kuwa nzuri kwani wengi wa wateja hapo hununua magari used toka kwa watumiaji wa DSM na mikoa mingine. Ukiwa serious nitakupa connection ya jamaa yangu mmoja yuko Dar ila uaminifu na commitment ni muhimu sana.Mhh ...nipo hapa hapa soweto na simfahamu huyo mtu ana yard ya magari??