Kama unamaanisha kweli na unataka kuifanya hiyo biashara, sitegemei utafanya maamuzi mazito ya kuwekeza kwa kuamini maneno ya hapa JF, hapa watu wote wanajua kila kitu lakini ukimuuliza mtu maswali ya msingi unaona kabisa hana uelewa na hajawahi kabisa kufanya kitu anachokielezea.
Ulizia hapo mtaani bei zikoje, nenda mashine wanazokoboa ulizia bei zikoje, fuatililia gharama za usafirishaji, kuhifadhi kisha upige mahesabu kama kuna faida. Kuna vitu lazima mwenyewe uchukue jukumu kupata habari za kuaminika na uhakika kabla ya kufanya maamuzi.
Ukipata muungwana anaefanya hiyo biashara akawa muwazi kukupa muongozo itapendeza sana.
carbamazepine