doriani
Member
- Nov 24, 2019
- 42
- 38
Nimeona ni vizuri niandike Makala hii ili waungwana akina Pascal Mayalla na wenzake wa some na waelewe ninachokusudia. Viongozi na waandishi wengi nchini mwetu huwa hawana dhamira njema ya kutaka kuwaeleza vijana wetu matokeo sahihi ya historia ya watu wa Oman na wananchi wa visiwa hivi vya Unguja na. Pemba. Nimeona Makala ya Pascal Mayalla akielezea Udhalimu wa Waarabu Unguja na Pemba.
Kwanza kabisa lazima mtu afahamu kwamba anapoweka uzito wa jiwe la mizani upande mmoja una tarajia nini matokeo ya mizani hiyo?. Hapana shaka itakua huna ulichokipima kwa vile hukuwekwa kitu upande wa Pili wa mizani.
Unapomueleza mtu ubaya wa Mwarabu na usimueleze mazuri yake aliyoyatenda ni sawasawa na kutoweka kitu upande wa Pili wa mezani. Sasa mimi natia kitu kidogo upande wa Pili kisha nimwachie Pascal apime atakavyo.
Katika Mwanzo wa karne ya 16 1503 Zanzibar ikapata msukosuko mkubwa wa Kwanza wa kuvamiwa na Wareno wa kaingia wakakalia Zanzibar.
Walienda kupiga Unguja Ukuu. Utawala huu ulikuwa ni utawala wa kuwadhalilisha na wakidhalimu kwa wananchi wa Zanzibar. Wananchi walipambana nao wakashindwa. Mateso yakawa makubwa Wareno walikuwa wakiwa Kata miguu na mikono wananchi wa Zanzibar na walizidisha unyama wao zaidi kwavile wengi wa wananchi wake walikuwa ni Waislamu. Mateso yao yalivyokuwa makubwa wakaamuwa kukusanya watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi hasa Unguja na Pemba.
Wakasema: Jamani hawa wazungu watatumaliza tufanyeje? Wakasema: Tume sikia katika nchi za Ghuba, kuna nchi ambayo imepambana na hawa wazungu (Wareno) na imewashinda nao ni Waoman kwanini hatuendi tukawaomba waje kutusaidia? Wakakubaliana wakatafuta jahazi wakapeleka Ujumbe kwenda kuomba msaada wakuja kumuindowa Mreno. Wakaja Waarabu wakapambana nao vizuri na mwishowe akashindwa.
NI jambo la kawaida kama umetafuta mtu na akakusaidia vita kisha wakashinda basi nae hubaki palepale na matokeo ya kubaki kwao waluowana na kuchanganya damu na kuzaliana nao watu wa Oman. Lakini ajabu hawa waandishi matokeo haya wao hawataki kuwaeleza vijana wao wala hayasomeshwi mashuleni kabisa ndio unapata waandishi wanaosomeshwa historia ya Zanzibar yenye mapengo mengi sana tena matokeo yake unakuja wapata kama hawa akina Pascal Mayalla.
Na ndio hayo hayo ya Mapinduzi ya Zanzibar waliwaita watu kutoka nje ya nchi wakaja kupinduwa na baada ya kupinduwa ndio wameikalia nchi watanganyika hadi leo. Amma hapa kwanza lazima tumshukuru Muoman kwa kumuondowa Mreno maana ingalikua tunaabudu masanamu ya Yesu na Maria na Misaraba majumbani mwetu kama vile huko India sehemu ya kisiwa cha Gowa.
Jambo la pili Waoman walitukubali na tukaozana nao na tukazaana nao kitendo ambacho kimetujengea daraja ya damu baina ya waswahili wa Unguja na Pemba kwa kzaana nao na ndio tukaitwa Waswahili maana hatuna lugha nyengine zaidi ya kiswahili angalau akina Pascal munazo lugha zenu za asili sisi hatuna zaidi ya hiyo.
Tusisahau kwamba Waarabu wengi waliuwawa katika kuja kutukombowa maana Mreno ni Taifa kubwa na lenye nguvu kubwa sana wakati huo wa karne ya 16.
Kauli za chuki zinazotumika dhidi ya Waraabu ni kauli zilizofundishwa na Wakoloni wa Kiingereza kwa kulitumia kanisa kueneza chuki zao dhidi ya Waarabu. Na hayo yote yamejiri sio kwasababu ya biashara ya Utumwa Hapana, maana utumwa hata wazungu na Waafrika walifanya sana tena zaidi hata kuwashinda Waarabu. Chuki zao ni dini maana Uislamu umekuja kufuta giza la dini ya Ukristo ambayo ni dini ya Wakoloni na watu kama hao akina Pascal.
Mimi hushangaa maana kila kitu kiko wazi ndani ya maandiko juu ya hustoria ya Utumwa. Hebu ukitupia macho Encyclopaedia of Religions jalada la ll, UK 602 inaelezea kwa kusema:katika mafunzo ya Mungu wetu hakupatikani kuchukia utumwa na hakuna hata dalili moja inayoonesha kuharamishwa utumwa.
Na katika Insight on the Scripture Vol ll UK 997 I aeleza hivi: For a Slave to have a Christian master was a blessing.
Basi ni vizuri tusiwapotoshe vijana wetu na tuwaelewe ukweli halafu wawe huru kudadisi na kutaka kujuwa ukweli. Hebu angalia leo watoto wetu hawajuwi kwamba Zanzibar iliopata Uhuru wake 1963.
Wala vijana wetu hawamjuwi Oscar Kambona ni nani alikuwa katika nchi hii, kichekesho Mkenya na MUINGEREZA wanayajuwa haya vizuri lakini watoto wetu ndani ya nchI yao wenyewe hawayajuwi zaidi ya "Udhalimu wa Waarabu Zanzibar".