BIG Africa
Member
- Oct 15, 2022
- 85
- 118
Habarini,
Naanza. Bila Shaka huwa unaona au kusikia kwamba soka au mpira wa miguu yaani "Football" ni biashara kubwa sana tangu miaka mingi. Unapona vilabu vikubwa kama Manchester United, FC Barcelona au PSG vinatumia pesa nyingi sana katika uwekezaji ndani na nje ya uwanja ujue pia vilabu na vyenyewe vinapata faida kubwa Sana. Sasa Hizo faida zinapatikanaje?
Zifuatazo ni njia mbalimbali ambazo vilabu mbalimbali duniani huzitumia kujipatia pesa
1. Mauzo ya mchezaji
Hapa vilabu hujipatia pesa Kwa kuuza wachezaji kwenda katika vilabu vingine vikubwa hasa wachezaji ambao Wana umri mdogo ambao Wana thamani kubwa na soko Lao ni kubwa.Mfano tazama jinsi Aston Villa walivyopata pesa nyingi (paund Mil 100) baada ya kuwa wamemuuza Jack Grealish kwenda Man City.Mifano ni mingi.
2. Kushiriki Michuano mbalimbali ya kimataifa na kitaifa ambapo timu hulipwa pesa "prize money"
Hapa ni hasa timu inapokuwa inafika hatua za juu za katika Michuano husika au kutwaa taji lenyewe. Mfano Simba ni mfano ya timu ya Tanzania ambayo imekuwa ikipata pesa nyingi kutoka CAF na hii inatokana na Mnyama kufika hatua za robo fainali mara Kwa mara.
3. Haki ya Matangazo ya Televisheni wazungu huita "TV Rights"
Hii pia ni njia nyingine ambayo timu nyingi duniani huzitumia kujipatia pesa. Hii ina maana kwamba mechi zote ambazo huwa unaziona live kwenye TV Timu husika huwa zinalipwa na Chombo cha habari husika. Mfano Kwa hapa Tanzania Azam Media ndio wanamiliki haki zote za kurusha Mechi zote live za Ligi Kuu NBC PL na Timu za Ligi Kuu zinalipwa pesa na Azam TV na habari njema ni kwamba miaka miwili iliyopita Azam TV waliongeza mzigo Kwa timu zote za Ligi Kuu
4. Kuingia mikataba ya kibiashara na makampuni mbalimbali yaani "endorsement"
Mfano ukiiona Yanga imevaa jezi yenye maneno SPORTS PESA kifuani ujue kampuni ya kubashiri ya Sports Pesa imeilipa pesa nyingi Yanga.Mifano ni mingi sana.
5. Viingilio vya uwanjani "Gate collections"
Mashabiki pindi wanapoingia uwanjani kuiangalia timu Yao ikicheza basi hulipa pesa na pesa hizo huenda moja Kwa moja Kwa vilabu. Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kila Klabu kuwa na Kiwanja chake kwani ni asset moja kubwa sana ya kuingizia mapato ya klabu na ndio maana Kwa wenzetu Ulaya timu huwa zinafanya maboresho ya viwanja vyao Kwa màana ya kuvitanua kuwa vikubwa zaidi lengo ni kuwa na idadi kubwa ya mashabiki kwani mashabiki wanapokuwa wengi zaidi uwanjani hivyo mapato ya klabu pia yanaongezeka.
6. Mauzo ya jezi pamoja na vifaa vingine vya michezo vyenye logo ya Klabu yaani "Merchandise"
Hapa kuna mawili. Jambo la Kwanza Klabu inaweza ikaamua yenyewe kuzalisha jezi na kuziuza moja Kwa moja Kwa mashabiki popote pale duniani. Au Jambo la pili Klabu inaweza ikaingia mkataba na kampuni ambayo itapewa haki ya kuzalisha jezi za Klabu husika na muda huo Kampuni inayozalisha jezi husika ikailipa Klabu pesa.Rejelea like ambacho kilifanywa na Fred VunjaBei na Simba.
MWISHO.