Biashara ya maharage - Tandika

Biashara ya maharage - Tandika

Codename96

Member
Joined
Sep 17, 2020
Posts
90
Reaction score
85
Habari za saa hizi wanachama wa jukwaa la biashara na ujasiriamali.

Nataka kufanya biashara ya kuuza maharage Tandika - dabo kibini ambapo ndipo lilipo soko la vyakula.

Mtaji wangu si mkubwa saaana lakini kwa hii biashara inawezekana kufanyika. Nina 1.1m.

Sasa nimekunja katika jukwaa hili kuomba uzoefu kutoka kwa wataalamu/wazoefu wa biashara za mazao/vyakula Tandika - dabo kibini.

1. Biashara huwa ipoje pale ? (mzunguko)

2. Wauzaji wa mazao/vyakula Tandika huwa wanatoa wapi mzigo ?, maana mtaji wangu ni mdogo sana kusafiri.

3. Kuna changamoto gani katika biashara hii ?

Natanguliza shukrani kwa mtu yeyote mwenye uzoefu kunipa mwongozo katika biashara hii. Asante.
 
Bora ungepita soko husika ukafanya kautafiti kidogo
 
Back
Top Bottom