Chunya Boy
New Member
- Nov 18, 2018
- 4
- 2
BIASHARA YA MAJI NI DILI
Siku chache zilizopita niweza kufanya mahojiano mafupi na bwana Athuman (si jina halisi) muuza maji kutoka mji mdogo wa madini Makongolosi Katika wilaya ya Chunya.
Na hii ndo historia ya maisha yake.
Bwana Athuman alizaliwa miaka ishirini na saba iliyopita katika wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Ni mtoto wa tatu kati ya sita kuzaliwa, katika familia yao yenye watoto wa kike wawili na waliobakia ni wa kiume.
Baada ya kumaliza Elimu ya msingi hakuweza kupata bahati ya kuendelea na Elimu ya juu kutokana na hali ya familia yao japo alichaguliwa kuendelea na kiwango hicho cha Elimu.
Aliamua kuondoka nyumbani kwao na kuelekea Wilayani Chunya katika mji huo wa Makongolosi baada ya kusikia kuna machimbo ya dhahabu hivyo niliona ni sehemu yangu kuingia machimboni ili nikifanikiwa niweze kuisaidia familia yangu.
"Nilipofika hapa mambo hayakuwa rahisi kama nilivyofikiria kwani nilikaa porini mimi na rafiki zangu tukifumua miamba kwa kipindi cha miezi miwili bila mafanikio." anasimulia.
Anasema hela waliyokuwa wanaipata ilikuwa kidogo sana ambayo iliishia kwenye pombe.
Anasema machimboni kuna changamoto nyingi sana kwani usipokuwa makini haurudi nyumbani salama. "Ukiwa machimboni utajifunza kuvuta bangi, kunywa pombe hasa pombe kali ya gongo ambayo huathiri mfumo mzima wa ubongo." Anasimulia.
Baada ya kuona kachakaa sana haeleweki aliamua kwenda kujisalimisha kwenye kanisa la Lutheran ambako alipata msaada wa kimaombezi na kuanzia hapo alianza maisha mapya.
Kwani aliachana na machimbo na kuanza kuuza maji biashara ambayo alishauriwa na rafiki yake.
Ni kweli alianza na dumu tatu na baiskeli aliyoazimwa na rafiki yake huyo.
Anaendelea kuwa mji wa Makongolosi una maji yenye asili ya chumvi, hivyo wengi hawayapendi. Yeye na rafiki yake waliingia kijiji cha Mkola kilometa chache kutoka hapo ambako kule kuna maji mazuri yasiyo na chumvi.
Hivyo walianza kuuza maji haya kwa bei ya shilingi 1000 kwa dumu hivyo kila safari moja alikuwa anaingiza shilingi 3000 kwa zile dumu tatu.
Na kwa siku alikuwa akienda safari 8 maana mwanzo ulikuwa mgumu. Hivyo aliingiza 3000 X 8 = 24,000/=
Akiondoa matumizi ya siku alikuwa anabakiwa na shilingi 10,000/=
Ndani ya miezi miwili ya mwanzo aliingiza shilingi 10,000 X 30 = 300,000 kwa mwezi na kwa miezi miwili alijikusanyia shilingi 600,000 ambayo ilimsaidia kutengeneza Mkokoteni wa kutosha dumu 10 ambazo hizi alizikopa miaka kadhaa nyuma kwa mama mmoja muuza genge.
Hivyo alianza safari mpya kutoka kwenye baiskeli mpaka kwenye Mkokoteni huu. Na kwa kutumia Mkokoteni aliweza kwenda safari 5 ambazo zilikuwa na wateja maalum.
Safari hizo 5 zilimwingizia kiasi cha shilingi 50,000 kwa mchanganuo huu.
Mkokoteni una dumu 10 kwa shilingi 1000 kwa dumu moja unapata shilingi 10,000 na ukienda safari 5 inakuwa Sawa na shilingi 50,000.
Anasema ameendelea na biashara hiyo mpaka sasa ni miaka 5 na Mkokoteni aliutumia kwa miaka 2 na kila siku ukiondoa matumizi yote alikuwa akihifadhi shilingi 30,000 kwa siku na mwezi una siku 30 ambayo inakupa shilingi 900,000 na mwaka una miezi 12 ambapo unakusanya shilingi 900,000 X 12 = 10800,000 (kwa mwaka) na kwa miaka 2 alivuna shilingi 21,600,000.
Kwa sasa Anasema anamiliki kajumba kake ameondoka kupanga. Ana miliki bodaboda tatu ambazo kila moja kwa mwezi inaingiza 300,000 na kwa zote tatu ni 900,000 na pia a nami liking Bajaj moja ambayo inaingiza 450,000 kwa mwezi na kwa siku ni elfu kumi na tano. MKOKOTENI ALIACHANA NAO.
Ametoa ajira kwa vijana wenzake.
Na kwa mwezi ana kusanya 1,350,000/=
MAFANIKIO ALIYOPATA MPAKA SASA
. KAOA NA ANA FAMILIA
. KAWAJENGEA NYUMBA WAZAZI WAKE
. KAMFUNGULIA DUKA LA VINYWAJI LAINI MKE WAKE (soda, juice na maji)
USHAURI WAKE
Usichague kazi wakati huna kazi na hauna uhakika na maisha yako.
NOTE.
PICHANI SI YEYE.
Na Chunya Boy.
Novemba, 2018