Biashara ya masaji inalipa?

Ushauri: Fungua Dodoma Mnadani lakini uweke mlango wa uwani!
 
Fungua eneo lenye privacy, mtu akienda huko asionekane kabisa.
 
hiyo biashara nzuri sana,hata mm ninampango huo coz nishapata chanel ya wateja bt sina uzoefu wa vifaa vyake na wafanyakazi jins ya kuwapata na malipo yao
 


Masaji ni nini? Ni nenolinalotumika kuelezea utalaam wa kunyumbua (kubonyeza, kusugua, kukanda) ngozina misuli ya mwili. Mtaalam wa masaji mara nyingi hutumia viganja vya mikono lakiniwanaweza kutumia sehemu nyingine za mwili kama vidole, viwiko hata miguu ilikuleta matokeo yanayohitajika. Pia kunavifaa mbalimbali vilivyotengenezwa kwa mbao, plastick na baadhi hutumia umeme.(kama vile electronic massage beds and chairs). Pamoja na vifaa vyote hivyo mikono ya binadamu ndio inasemekana kuleta matokeo mazuri zaidi. Hii ni taaluma ambayo ipo tangu enzi na sehemu nyingine katika nchi zaAsia unakuta kila familia ina angalau mtu mmoja anayeweza kuifanya kazi hii kwa ustadi.Nimewahi kusikia sehemu za Zanzibar wakiwaita Β“wakandaji.





Masaji imewekwa kwenye kundi la tiba mbadala ingawa imekuwa ikitumika hata kwenye tiba za kisasa (katika hospitali n.k). Biashara ya masaji ikijumishwa na biashara nyingine za Β‘WellnessΒ” ni ya mabilioni ya dola vikiwemo vifaa, mavazi ya wahudumu, mifumo ya kompyuta kwa ajili ya usimamizi wa senta na mafuta mbalimbali ya kiasili ambayo hutumika. Nchi nyingine tiba ya masaji imeongezwa kwenye bima za afya na imekuwa ikipendekezwa na madaktari. Taaluma ya masaji imekuasana kwa sasa ambapo kuna masaji maalum kwa ajili ya vichanga na wajamwazito. Kwa mfumo wa maisha ulivyo sasa na pia kutokanana kukua kwa vipato ni dhahiri biashara ya masaji itaendelea kushamiri na kuwa muhimu katika maisha ya kila siku.





Faida za masaji: Masaji ina faida nyingi mwilini moja kuu ni husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini na kupelekea kutibu hali mbalimbali hasa msongowa mawazo na msongo wa misuli.


Navyoiona biashara ya masaji Tanzania: Kwanza inakua kwa kasi, sasa hivi hoteli nyingi kisasa zina vitengo vya masaji. Huko angalau kuna utaratibu na ustaarabu unaotakiwa na wahudumu wana utaalaam/ elimu kuhusu masaji. Lakini pia naona kuongezeka kwa watu wanaotambua umuhimu wa masaji na wanaoweza kutoa hela ili wapate huduma hii. (Massage is not cheap).


Ukiondoa sehemu ya hali ya juu, huku kwingine tumekuwa na sehemu za masaji ambazo baadhi zinajitahidi kuwa za kitaalam ila nyingi zinalalamikiwa kutumiwa kama mlango wa biashara nyingine. Masaji ni taaluma, unahitaji kwenda shule ile ufahamu unachokifanya kwenye mwili wa binadamu kujua misuli ya mwili, milalo nakazi zake. Mara nyingi kazi ya masaji imefananishwa kama tu kitu cha kuonyeshwa halafu unajua (look and do), hapana. Kwa hiyo bado suala la kuwa mfumo wa kuandaa wataalam hawa hatunao .Na kwa kukosekana taaluma hii pia tunaona mapungufu makubwa katika masharti kwa watoaji wa huduma hii. Unakuta mhudumu amefuga kucha refu, amevaa mavazi yanayoonyesha sehemu za mwili wake n.k. Katika nchi zilizoendelea wataalam wa masaji (massage technicians, massage therapists wamekuwa wakilinda sana taaluma yao kwa kuweka masharti ambayo hufuatwa na kila mmoja wao. Kuna utitiri wa watu wanaotoa huduma hii ndivyo sivyo- quacks).


Ushauri kwa wanaoona fursa ya kibiashara


1. Eneo lako la biashara liwe mahali ambapo ni pa kuaminika sio vichochoroni. (kwa mfano uwe na ample parking na security)


2. Gharamia muonekano wa kitu chako cha masaji (muonekano, vifaa, vitanda, sehemu ya kusubiri wateja). Weka mandhari nzuri ndani ya vyumba, decorate pawe na reception ambayo mteja atakuwa huru kusubiri. Pia uwe na receptionist anayeweza kupokea appointments za wateja.


3.Vyumba viwe na mpangilio mzuri,vifaa visafi shuka na mataulo. Pia hakikisha unaweka vitanda vile maalum kwaajili ya masaji kama vinavyoonekana kwenye picha.








Vyumba viwe nadhifu.











4. Toa mafunzo kwa wahudumu wako,(angalau wajue basics za masaji), wawe na mavazi maalum ya kazi na pia sisitizaunadhifu. Sehemu nyingine hutoa mikataba na kuwapa sheria ya kutojiusisha namahusiano yoyote mabaya na wateja.Wengine wameenda mbali wamefunga surveillancecameras kufuatilia mienendo ya staff wao wakiwa kazini.





Hawa wahudumu wa picha ya juu napicha ya chini. Tofautisha pia aina ya vitanda vilivyotumika kwenye picha yachini. (Biashara za masaji kuchanganywa na biashara ya ngono imekuwa tatizokubwa.)





Upande wa pili wa wateja wamasaji nao unatakiwa uangaliwe kwa umakini. Watu wengi wa mtizamo kuwa sehemuzinazotoa huduma za masaji pia ni madanguro. Ni muhimu wateja wako wakawa na uelewa sahihiwa huduma unayotoa. Wakati mwinginesenta zimekuwa zikiotoa waraka ambao mteja anasaini kwamba yupo kwa ajili yahuduma masaji tu. Kwa sababu hutokea baadhiya wateja kuwalazimisha wahudumu kuwashika sehemu za siri au hata kufanya naowapenzi. (Wahudumu inabidi walindwepia).





Session ya masaji inawezakuchukua kuanzia dk 15 mpaka 90 kutegemea na eneo la mwili. Inaweza kuwa mikono , miguu, mgongo au mwilimzima.





Natumaini haya machache yanawezakukusaidia Ndg LIKUD. Naweza kujibu kamauna maswali ya ziada.




 
DorothyMankaa picha zako mbona azionekani kabisaa. .nimependa sanaa comments yako
 
Inauzwa bei ngapi
 

Attachments

  • 1422778111827.jpg
    8.7 KB · Views: 149
Masaji na danguro ni kama chanda na pete!

Hii ni misconception. Kwa wale wanaojua professional massage ni kama tiba. Jaribu tu ku google "massage business USA".Wenzetu huko wana kada kabisa iliyosajiliwa "massage therapists/ massagists".
 
hii kitu inalipa sana ila kwa wabongo tulio wengi tunaiona kama haram coz mtu akipigwa ile hard massage atatoka hapo akiwa ... na kutaka apate mchepuko wa kwenda nao. nachojua mimi kuhusu vifaa naonaga towels, kitanda maalumu kwa kazi hiyo, almond oil, yapo mafuta ya aina tofauti tofauti ila hii almond ndio hutumika kwa wingi kwenye hizi 5 star hotel's pia kuhusu masseuses wapo kibao miji ya mombasa na malindi kenya. Thanks
 

Kaka we. Mkali
 
pure massage...complete massage....full massage...massage with happy ending....etc. yako itakuwa ya aina gani?!!!
 
pure massage...complete massage....full massage...massage with happy ending....etc. yako itakuwa ya aina gani?!!!

Massage with happy endingπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…