OllaChuga Oc
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 21,569
- 24,812
Wakuu khabari za asubuhi, mimi kijana wenu mpambanaji ..naendelea kutafuta ni kwa namna gani naweza kujiongezèa kipato. Katika pita pita za town naona kuna fursa ya kufanya hii biashara ya matunda mchanganyiko au kachumbari ya matunda (fruit Salad). Nipeni muongozo wakubwa, naomba kujua changamoto zake, mfano upatikanaji wa matunda, vifungashio, maana nataka nifanye kwa mtindo flani hivi wa kisasa.
Soko langu nimelenga watu wa maofisi, hospital na hata viwandani ila sjajua nitumie approach gani kufikia hao wateja, yani kuwatangazia. Je niende na product kabisa niwaoneshe au niende mikono mitupu au niandae vipeperushi then nipitishe maeneo mbali mbali kwa ajili ya kuwaonesha? Mimi nipo Arusha kwa sasa na nitakuwa nafanya supply kwa order nitakazopata.
Mpaka sasa nimenunua friji na bado natafuta vifungashio ikiwa pamoja na zile umma za plastic pamoja na tissue. Lengo nifanye biz iwe na muonekano Mzuri. Je ni wakati gani niwaendee wateja? Wakati wa asubuhi au mchana? Nitumie mbinu gani ili niweze kuliteka solo na kupata wateja wa uhakika?
Nakaribisha mawazo yenu wakuu.