Biashara ya matunda nje ya nchi

Saleko

Senior Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
128
Reaction score
67
Wana jf,mim ni mfanyabiashara mdogo,sasa hivi karibuni kuna ndg yangu kanipa deal ya kuuza matunda nje ya nchi hasa Dubai,naomba kwa wanaofahamu wanipe muongozo wa biashara hii na jinsi ninavyoweza kuyapata haya matunda kwa urahisi!matunda yenyewe ni Maembe,Machungwa,Mananasi na mengeneyo!!AHSANTENI!!
 
Mimi ninashamba la mananasi huko rufiji/kijiji hanga km 150 kutoka dar nina uwezo wa kujaza contena ft20 kuanzia mwezi wa 12 tarehe 18hivi na kuendelea hadi jaruar 27,uwezo huo upo nabado sijapata mteja pamanent, kwa malezo zaidi wasiliana na namba hizi 0787334714,0782138541
 


Wazo lako ni zuri sana na kwa mtu anayetegemea maendeleo hii ni fursa.
Hatua ya kuamua kusafirisha matunda/chakula ktk nchi zilizoendelea ni suala la kisheria mkuu.
Nchi zilizoendelea zina sera za uzalishaji pamoja na viwango vyake katika imported ya chakula kama matunda.
Kule katika mataifa yaliyoendelea kuna baadhi ya inchi ambazo hazipokei chochote kutoka nje ya inchi.
Afrika kwa bahati mbaya tumekua ni bara ambalo nchi zilizoendelea huuza bidhaa zao ikiwemo matunda, ni mara chache sana sana kwa nchi zilizoendelea kuinported mzigo wa chakula kutoka nje,
Sikukatishi tamaa lakini ukweli ni kuwa sera za ulaya na magharibi ni kuuza bidhaa africa, sasa wakiruhusu africa kuuza chakula ulaya na mash-kati huoni soko lao litakufa ,maana africa hawatanunua tena na viongozi wa rasi ya eneo hilo hawatakubali kutokea kitu kama hicho.
Ni heri ungeangalia soko hapa karibu na nyumbani.
Mfano.Kenya,South africa,Zimbabwe na Ethiopia
 
Mkuu nikukosoe kidogo, Ni kweli inaweza kuwa ngumu kusafirisha mazao ya vyakula, lakini hizo pande za dunia ulizotaja nyingi zao hata muhogo haumei, mara nyingi matunda na mazao mengi ya misosi wanatoa kutoka nchi tofauti za latin america na mengine spain, Africa pia tunapeleka sana mazao yetu huko kwa *THE YES PLEASE' sijui kama apo humu lakini wakulima wengi wanarusha mazao yao ulaya. kenya ndio usiseme, tani na tani ziainuka kila siku. Ila tu Ni kweli ugumu wake unakuja pale kwenye kukamilisha na kufuata sheria zao. kwa mtazamo wangu mimi, kama mtu anaweza kudili na huu usumbufu tunaoupata hapa nchini kwetu kwa kuendeleza taifa, basi hiyo ya ulaya haitomshinda kwa sababu kule usumbufu na maringo maofisini hakuna. angalau sio kama yalivyozidi hapa kwetu
 

si kweli matunda na vyakula kama ndizi ambazo viko marekan vinatoka uganda na jamaica. tatizo la watanzania atuchangamkii fursa.
majiran zetu kenya na uganda wanachangamkia. Africa atuwez kuuza nje electronics au magari kwa vile atutengenez lakin chakula kama matunda tunaweza.

Kuna kitu kinaitwa AGOA watz wengi awajui hiyo ilianzishwa na marekan kusaidia wafanyabiashara ndogo ndogo watokao nchi masikin kama Africa kuuza bidhaa zao marekan bila kukatwa kodi.

mim uwa nawaona wakenya, waganda, na wengine wakitumia fursa hiyo watanzania tunatishana pia hakuna elimu nzuri kujua bidhaa gani zina soko ulaya, marekani na uarabuni.

pia watanzania ni waoga wa kuthubutu
 


Vizuri sana kwa maana na wewe umeonyesha mbadala wa hio fursa, cha msingi sasa ni huyu aliyeleta thread kuifatilia hio Ng,o ili kufanikisha hayo mazao
 
inataka utafiti wa soko na viwango nilisha jaribu kufanya utafiti .kuna senta ya biashara Dubai na uingereza zote watakupa mwongozo nini cha kufanya maana zipo kwenye balozi zetu.
 
mwenye thread ameuliza jinsi ya kupata mzigo tu, mchongo wa soko tayari anao, sasa nyie mnakuja na siasa nyiiingi! uko wapi lucky sabasaba jamaa anataka kuleta bidhaa huko jamaa wanamtisha! Malila mzee wa shamba msaada wako unahitajika huku!
 
Last edited by a moderator:
inataka utafiti wa soko na viwango nilisha jaribu kufanya utafiti .kuna senta ya biashara Dubai na uingereza zote watakupa mwongozo nini cha kufanya maana zipo kwenye balozi zetu.

Mkuu unaonaje ukifunguka Zaidi khs utafiti uliofanya naamini Utasaidia wengi hapa Jukwaani!
 
Ku Export matunda nje ni ishu ngumu sana, si swala la kitoto hata siku moja, ku meet standard yao ni kazi kubwa sana ingawa inawezekana, Ila ni mpaka uwe na maandalizi ya muda mrefu, jamaa wako makini sana na maswala ya afya za wananchi wao.
Kwanza ni lazima wewe uwe na shamba lako mwenyewe ambalo utaweza ku maintaine viwango, huwezi kamwe ukawa unaenda kupkota matunda kwenye mashamba ya watu utegemee kuyauza Ulaya au Asia,

Ni lazima upate kibari au ithibitishwe na TBS ya bongo na bado mashirika ya viwango ya nchi husika, wanapima sample kukujua aina ya madawa unayo tumia, mbolea na kazalika.

Hapo bado hujaingia kwenye kushindana na wazalishaji kutoka mataifa mengine

Anzeni kwanza kuuza ndani ili kupata uzoefu na ni lazima wewe uwe mzalishaji mkuu na si dalali.
 
Mkuu unaonaje ukifunguka Zaidi khs utafiti uliofanya naamini Utasaidia wengi hapa Jukwaani!

kama uarabuni matunda ni biashara kubwa ila kuna viwango mfano Maembe kuna aina wanazi hitaji na kuna aina ya uandaji kuna madawa ya kupiga ili ziwe kwenye kiwango chao.
Niproject kwakua pengine uwe na shamba uzalishe mwenyewe au utoe elimu Kwa wakulima wazalishe wewe ununue kutoka kwao.
sema maelezo ni marefu siwezi kuandika yote.
uni pm nikupe maelezo ya kutosha
 
mwenye thread ameuliza jinsi ya kupata mzigo tu, mchongo wa soko tayari anao, sasa nyie mnakuja na siasa nyiiingi! uko wapi lucky sabasaba jamaa anataka kuleta bidhaa huko jamaa wanamtisha! Malila mzee wa shamba msaada wako unahitajika huku!

Nilikuwa shamba Njombe,
Ni kweli soko la Ulaya linataka viwango ila lipo na linakuwa sana. Wapo vijana njombe wanauza parachichi Italy, na mimi nimefika shambani kwao. Nikiwa Njombe mjini nimeshuhudia maandalizi ya kilimo cha Matunda kule Ihanga,pia Madeke Lupembe kuna nanasi la kufa mtu na kiwanda kinajengwa. Kwa sasa parachichi zinasindikwa Kiwira Mby, akina Chai bora wanalima parachichi for export kule Mby/Mufindi.

Kwa ufupi, soko la matunda huko majuu lipo sana toka huku kwetu, kama mtu yuko serious aseme nimpe simu ya vijana pale njombe aone nini kinaendelea.


Ni vizuri kujua mteja anataka viwango gani na wewe utimize,usichakachue. Nikiwa Iringa ktk kiwanda fulani, Waholanzi walimwaga mzigo wetu wote baharini kwa sababu tuliongeza sukari kidogo ktk pineapple rings tulizopeleka.
 
Huu uzi mzuri sana,naomba wenye uzoefu zaidi mzidi kutoa ushauri wenu hapa.
 
Wonderful thread. Vipi bidhaa kama mafuta ya Alizeti, Asali na karanga??
 
Naomba kuwasiliana na wewe mkuu
 
WEWE WAONESHA KUWA UNA KITU CHA KUJIFUNZA KWAKO NAOMBA UNIPE ADDRESS ZA HAO VIJANA NAMI NIIKAWAULIZE NAMNA YA KUFANYA BIASHARA HIYO NJE YA NCHI
 
NAOMBA MAWASILIANO NA HAO VIJANA WA NJOMBE PLS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…