Biashara ya mawe

Kashaija72

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2020
Posts
2,225
Reaction score
5,258
Kwa muda mrefu sasa, nimekuwa naona jinsi watu wanavyohangaika kutafuta mawe ya kujengea misingi ya nyumba, viwanda masoko, mitaro n.k.

Kwenye baadhi ya miji, upatikanaji wa mawe ni wa shida sana mpaka wajenzi wanatumia tofari tu kujenga msingi.

Tangu miaka mitatu iliyopita nilikuwa nawaza jinsi gani naweza kuingia kwenye biashara, kwa kuiboresha na kuwahakikishia wateja upatikanaji wa mawe kwa misimu yote na mahali ambapo sio mbali kutoka mjini, kwa bei nzuri. Kwa sasa mawe huokotwa milimani, husogezwa mpaka eneo la kupakilia. Mawe ya kuokota hayana ubora Sana, mengi yanamung'unyika, muda mwingine mawe madogo yanazidi makubwa na yanapatikana mbali kwa msimu.

Katika kufanya utafiti wa hapa na pale, nikaja kufahamu kuhusu uwepo wa chemicals za kupasua miamba na mawe bila kutumia vilipuzi.
Betonamit, Dexpan na Becker ni baadhi ya non-explosive cracking agents. Sina taarifa Kama hizo chemicals zinapatikana hapa Tanzania na kwa Bei gani.

Hapa nilipo, trip ya mawe inauzwa 70,000 (wakusanya mawe wanachukua 40,000 na mwenye gari anachukua 30,000).

Naomba mwenye uelewa wa hizo chemicals kuhusu upatikanaji wake nchini, Bei zake na matumizi yake (zikitumika kupasulia mawe italeta faida au la).
Je process za ku-import chemicals zipoje?
Pia nakaribisha mawazo ya kiuwekezaji.
 
Hizo chemicals sijui Kama zipo Tanzania. Labda nikuletee toka nje
 
vipi hizo chemicals zimeshafika bongo wakuu ?
 
Kwa hiyo mtu akianzisha kiwanda au mradi wa kuchakata mawe ili kuleta huku dar es salaam atapata faida? Maana nashangaa sana watu wanatumia tofali kujenga msingi wa nyumba zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…