Biashara ya mazao Oman

Biashara ya mazao Oman

shafii77

Member
Joined
Mar 18, 2019
Posts
60
Reaction score
85
Kuna fulsa nimeiona Oman, ya kupeleka maharage soya na Matunda pashen, nafikilia kuanza kupeleka bidhaa tajwa hapo juu kila week, kwa kuanzia ntakua nasafirisha kilo 100 kila week.

Kama unafanya kazi kwenye Kampuni za Ndege hasa zinazoruka direct toka Dar es salaam to Muscat, au unafanya biashara Kama hii hata iwe ni kwa other Gulf countries, uzoefu wowote, ntashukuru ukitoa uzoefu wako.

*Napenda kujua gharama za kusafirisha mzigo.
*Changamoto n.k

Shukrani!
 
Tafuta forwarding agent yeyote atakusaidia. Kuexport si complex sana kama watu wanavyofikiri..

Hakikisha una standard certification ya bidhaa unazotaka kuexport, pia ni vyema ukaenda nchi unayotaka kufanya biashara nayo ukajia standard zao zilivyo na taratibu zao za kuimport kutoka nchi nyengine.

Airline zipo nyingi na zinazotoka Tanzania kwenda nje zina nafasi kubwa tu. Ila ningekushauri kwa mizigo mikubwa tumia meli tu na refrigirated containers biashara ikichangamka
 
Shukrani sana ndugu, Ila ishu ya kutumia meli ni ngumu mno kwa sababu inagharimu muda mwingi sana na Kuna risk ya mzgo kufika umeharikiba mfano hayo matunda hayapaswi kuzidi siku5 yawe yamefika
 
Unapopeleka huko hizo bidhaa inabidi kwanza ipimwe maabara kisha content wanazotaka zikiwa sawa ndio usafirishe au wao watakupa standard ya bidhaa wanayotaka na uweke kwenye packaging ipi.

Lazima uweke Certificate of Origin, hii utaipata pale Tanzania Chambers of Commerce kuonyesha bidhaa imezalishwa Tanzania.

Phytosanitary Certificate utapata wizara ya kilimo kuonyesha mzigo ni msafi na salama kwa binadamu.

Quality Certificate utapata maabara utayopeleka sampuli kupimwa.

Packing list, Airway bill of lading au Bill of Lading itaandaliwa baada ya mzigo kuwa tayari kusafirishwa. Clearing Agent ndio atakaye kusaidia kusafirisha mzigo na utatakiwa kulipa kodi na gharama za kusafirisha mzigo wako
 
Kuna siku niliwahi kufikiria Kwa Nini Bakhresa asinunue boti itakayoweza kutumiwa na wafanya biashara kupeleka matunda nchi za Kiarabu

Unajua haya mambo ya ndege wengine wanaona shida
 
Kuna siku niliwahi kufikiria Kwa Nini Bakhresa asinunue boti itakayoweza kutumiwa na wafanya biashara kupeleka matunda nchi za Kiarabu

Unajua haya mambo ya ndege wengine wanaona shida
Boti? Boti boti au? Umesema boti ipeleke bidhaa nchi za kiarabu. Zipi hizo ulifikiria?
 
Kama unazo nyingi jaribu kwenye viwanda vya vyama unaweza ukapata pakuazia, au viwanda vya soseji maana niliona uganda kuna soseji za nyama ya bata.
 
Back
Top Bottom