Technolojia inapatikana na mashine zinapatikana ila vyote vinategemea na uwezo wako wa kuzalisha. Yaani unataka technolojia na mashine ya ku process lita ngapi kwa siku au saa. maana kama unazungumzia chini ya lita 100 au una uwezo wa kuzalisha/kukusanya zaidi ya lita 1000 nk.
Kwa mfano unaweza ukachemsha maziwa kwenye joto dogo (63 C) kwa dak 15 au (72 C kwa sek 16), maziwa hayo yanaweza kukaa kwa siku 7 hadi 14 bila kuharibika kwenye ubaridi siyo freezer.
Unaweza ukatumia joto kali (120 C kwa sekunde 10) alafu ukapaki kwenye chombo kisafi, ambacho hakipitishi hewa na hakina hewa ndani, yakakaa kwa muda wa miezi 6 hadi mwaka 1 bila kuweka kwenye friji. Hii ni technolojia ya hali ya juu kidogo