Biashara ya mbao za mitiki

Biashara ya mbao za mitiki

frozen

Senior Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
135
Reaction score
32
Wadau salam zangu za dhati kwenu,

Nataka kufanya biashara ya mbao za miti kwa hapa Dar es salaam, lakini sina taarifa za kutosha kuhusu soko lake na bei zake kiujumla, ntafurahi kupata taarifa zidi kwa yeyeto ambaye ameshawahi au anafanya biashara ya mbao hapa Dar es salaam;

i. Bei za mbao za mitiki
ii. Maeneo hapa dar es salaam ambako wanatumia sana mbao za mitiki katika kutengeneza furniture na bidhaa zingine
ii. Maeneo gani wanauza mbao za mitiki kwa hapa dar es salaam.

Natumai mchango wenu katika kupata taarifa zaidi kuhusu biashara ya mbao za mitiki hapa dar.

Asante
 
Mbao za Mitiki hazina soko sana hapa Tanzania. Soko lake kubwa lipo nchi za nje kama India na Dubai. Mimi ninalo soko kubwa la mbao za Teak hadi kontena 40 kwa mwezi. Je, miti yako ina umri gani? Na unauza dola ngapi kwa CBM? Na ipo wapi? Je, ni ya shamba la serikali au binafsi? Jumla unazo CBM ngapi? Na kwa mwezi unaweza kuandaa CBM ngapi? Ni PM hayo majibu ili nikupe vipimo tufanye biashara.
 
Naomba nipigie nami nina mitiki mingi Kibaha.
Ben mobile 0754 868 204
 
Back
Top Bottom