Kuna sehemu nilikuja maeneo ya Arusha panaitwa Lokii tukamkuta jamaa anachunga Mbuzi ni wake mwenyewe, ikawa kama tunaulizia tu aisee Mbuzi kama huyu ni bei gani, jamaa akasema huyo ni 30 na huyu ni 40 aisee tulishangaa sana. Huyo Mbuzi wa 40 kwa Dar huwezi kumpata chini ya 80 ikishuka saaaaana basi 70.
Niliitamani sana hii biashara japokuwa huyo ni mfugaji lakini huwa kunakuwa na mnada nafkiri ni kila siku ya Ijumaa japo sikuwahi kufika mnadani coz haikuwa Ijumaa na pia tulienda kwa ajili ya research na wanafunzi WA chuo.