nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,902
- 2,488
Unamlipa au anajilipa?Kwa jiko la chipsi gesi ina unafuu zaidi kwa sababu unaiwasha pale unapotumia tu ukimaliza unaizima. Tofauti na mkaa ambao utalazimika kuiwasha na kuongeza muda wote hata ambapo hupiki ili mradi moto uwepo.
Kuhusu malipo jiko la chips wanalipwa kuanzia 5000 mpaka 10000 inategemea na masaa anayokuwepo kazini, je ana usaidizi au yupo mwenyewe. Ingawa sana sana malipo ni 5000 au 7000
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa wabobezi wa kuuza chips wanajua kabisa debe moja la viazi linatoa sahani ngapi. Ukishajua hilo basi hata ukimwachia biashara hautapata shida kujua alichouza na anachokukabidhi ili mradi uwe na ufwatiliaji kwa karibu.Unamlipa au anajilipa?
Maana unamuachia biashara wewe haupo inakuaje kiasi atakachokupa kuwa ndicho alichouza?