bunyebunye
JF-Expert Member
- Apr 12, 2013
- 530
- 676
Salaam wakuu.
Nimekuwa na wazo la kuanzisha utengenezaji wa mishumaa iliyowekewa dawa inayofukuza mbu. Nimefuatilia baadhi video youtube zinazoonyesha namna ya kutengeneza mishumaa nikajifunza na kufanya majaribio kwa kununua mishumaa nikaiyeyusha na kutengeneza mshumaa mmoja wenye umbo kubwa tofauti na ile niliyonunua pia nilipouwasha ukawaka vizuri.
Mimi niko mkoani hivyo nategemea kuanza kutengeneza na kuuza kwa kutembeza vijijini ambako bado hakuna huduma ya umeme. Lakini pia nitauza mijini kwasababu mishumaa hii itakuwa na dawa ya kufukuza mbu.
Naomba mawazo kutoka kwa yeyote aliye na uelewa wa biashara hii, changamoto zake na mbinu za kutumia ili niweze kufanikisha wazo hili.
Asanteni na karibuni.