Naomba kujua kuhusu bishara ya miti yambao Iringa. Ninataka kununua shamba ili nipande miti then baadae nije kuiuza. Nilichokuwa nataka kujua ni...
*Je, huwa inachukua miaka mingapi?
*Bei ya kila mti ni shillingi ngapi?
*Na pia gharama zingine kama zipo
*Na weza nikaanza na heka ngapi
Kuhusu kununua eneo gharama hakuna tatizo. Naombeni msaada kwa wale wanaoifanya shughuli hii.
Nimeifanya biashara ya mbao na magogo kwa miaka Kama 4 hivi.
Miti inauolimwa Sana ni Pine(msindano) na eucalyptus (mlingoti)
Pine
Mche unauzwa 100-200
Ekari 1 inachukua Miche 550-650
Unatakiwa kuihudumia kwa miaka yote mpaka unavuna. Hapa ni kuweka barabara ya kuzuia moto kuzunguka shamba Zima+kukatia matawi mara 2 mpaka kuvuna. Usisahau kupunguzia(thinning) mwaka wa 6 au 7.
Ukitaka ikulipe vizuri inashauriwa itunze mpaka mwaka wa 14 au zaidi. Kwa umri huo unao uhakika wa kuuza 5000-8000 kwa mti mmoja.
Ukivuna mara moja unayokazi ya kupanda mingine tena.
Mlingoti
Mche unauzwa 150-300
Ekari 1 inachukua Miche 650-800 (inabananishwa ili irefuke zaidi).
Utaihudumia kwa miaka 5 ya mwanzoni baada ya hapo unaiacha. Huduma yake hapo ni barabara ya kuzuia moto tu. Hii haikatiwi matawi maana huwa inajipruni yenyewe.
Mwaka wa 8 unaweza kuvuna nguzo ambazo bei huwa ni 15000-30000 kutegemea zilipo. Au ukivumilia mwaka 15 na kuendelea unauza kwa ajili ya mbao. Mti mmoja huuzwa Kati ya 40,000 -100,000 kwa mti mmoja.
Ikishavunwa inaota mingine kutoka kwenye visiki hivyo, utavuna wewe mpaka mjuu wako atavuna pia.
Usiangalie muda wa kuihudumia, angalia utakuja kupata nini na ni lini.
Kila la kheri mkuu.