Rodgers Bernard
Member
- Oct 14, 2018
- 66
- 63
Mkuu hiyo biashara kama hujawahi kuifanya ni kujitoa mhanga tu, kwani tatizo liko kwenye uchaguaji, wa mpunga, kwani inahitaji uzoefu sana, ukikosea tu ni hasara kubwa sana, ambayo itakuja tokea, kwani unaweza kuja kuukoboa, ukakatika katika sana, ukakuta hata bei tu ya manunuzi isirudi!!, au ukanunua BIRIANI(Mpunga uliotunzwa vibaya ukavunda) hiyo ndio balaaa, kuuza ni ngumu, bora biashara ya mchele tu.
Halafu unaweza ukaununua kwa hiyo 45,000 hadi uufikishe store, ukafikia kwenye 60,000!! Ukauweka, ukisubiria bei ipande, ikakataa, biashara ya mazao huwa ni bahati tu, huoni mahindi, wamepata hasara sana watu huko, nyuma, mwaka jana ikawa neema kwao?
Mpunga ni pasua kichwa, kuna wazoefu wake, akiushika tu na mkono, akausugua anakwambia huu, ni mmoja mmoja. Na kweli ukikoboa tu ni hivyo hivyo
Nimemuuliza mtaalam wa mishe za mpunga kaniambia kuwa mwaka huu mvua nyingi. Mpunga utakuwa mwingi sana na hivyo bei haitapanda na inaweza kushuka zaidi.
Labda kama una mtaji mkubwa uukoboe mpunga upate mchele kisha ujaze scania semi (gunia 200) upeleke Kenya na Uganda. Ila inabidi uwe makini maana wakenya wakiona mchele haupo serikali inaruhusu watu kuagiza mchele hata mbovu uingie kenya.Huu mwaka ni kukusanya na kula tu🤧
Labda kama una mtaji mkubwa uukoboe mpunga upate mchele kisha ujaze scania semi (gunia 200) upeleke Kenya na Uganda. Ila inabidi uwe makini maana wakenya wakiona mchele haupo serikali inaruhusu watu kuagiza mchele hata mbovu uingie kenya.
Wenye mijihela yao wanakuwa wanaona kawaida. Nahisi gharama ni kati ya 30m mpaka 40m kwa semi la scania kulijaza mchele. Ila faida wanapata maana kilo ya mchele kenya ni kati ya 2500 mpaka 3500.Wenye mitaji yao