Biashara ya msimu: Nini cha kuzingatia?

Kipilipili

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2010
Posts
2,272
Reaction score
1,897
Habari!

Je biashara yako ni ya aina gani?

Je ni biashara ambayo huwezi kuifanya katika muda wote wa mwaka? ikiwa jibu ni NDIYO, basi biashara yako ni ya MSIMU.

Je msimu wa biashara unapokwisha(kipindi mauzo yanapokuwa madogo)unafanya nini?

Haya ni mambo muhimu ya k​uzingatia;

1. Dhibiti mtiririko wako wa pesa vizuri(cash flow management)

2. Punguza matumizi (expenditures)

3. Usiajiri wafanyakazi wapya.

4. Kuwa na mikataba ya muda mfupi na wafanyakazi wako, ukilenga mwisho wa mkataba uwe ni kipindi msimu unapomalizikia. Ishi na wafanyakazi hao vizuri, ili uweze kuwaajiri tena msimu unapoanza ili kuepuka gharama kuajiri "watu wapya" kabisa ambapo utahitaji gharama kubwa kuwa-train.

5. Fanya store management, hakikisha unajuwa kilichopo store: kiasi gani kipo, expire date. Hii itasaidia kuepukana na hasara.

6. Jitahidi kuweka akiba hasa kipindi biashara inapokuwa nzuri(boom stage). Akiba hii unaweza kuitumia kuinvest kitu kingine kipindi msimu wa biashara unapokwisha.

7. Hakikisha unadumisha mawasiliano na wateja wako katika kipindi kisicho cha msimu ili msimu unaporudi usianze moja kutafuta wateja.

8. Wakati unapoona msimu unakaribia kwisha , anzisha biashara ndogo ndogo ambayo ina uhusiano na biashara yako kuu au isiyo na uhusiano. Mfano kama unauza vinywaji baridi, unapokaribia msimu wa mvua huwezi kuendelea kuuza vinywaji baridi ila unaweza kuweka vitafunwa(bites), kuuza chips, chai nk. hii sionekane kuwa una- diverge from the core business ila ni kuweka altenative.

Jiulize kama unauza hoteli halafu imani yako haikuruhusu kuuza chakula mwezi wa ramadhani mchana, je utafunga biashara mwezi mzima? Nina mfano wa mgahawa mmoja uko pale kariakoo msimbazi karibu na Big bon, ikifika mwezi wa ramadhani wanauza nguo, ramadhani ikiisha wanarudi kwenye biashara yao ya chakula.

8.Ukiwa ndio unaanza biashara, na biashara yako ni ya msimu, Fanya forecasting kwa kuangalia data za mauzo kutoka kwa marafiki au watu wafanyao biashara kama hiyo. hii itasaidia kujua ununue mzigo wa kiasi gani ambao utauuza hadi mwisho wa msimu bila kubakia na kuingia hasara.

9.................

NB: Haya ni maoni yangu, I stand to be corrected! Tips hizi hazikupi guarantee ya kuwa succsesful business person, za kuambiwa changanya na zako..

Nawatakia weekend njema na biashara njema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…