Biashara ya mtumba, mtaji laki sita, (mauzo chini 4m). Nifanyeje kuepuka usumbufu wa watendaji?

Sijui umeandika vitu gani yaani utadhani ulikuwa unachat na mtu halafu umecopy conversation ukapaste hapa. Yaani umepuyanga kwa kifupi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ndugu, we kipi hujaelewa hapo, kwa elimu yako unataka ueleweshwe kama mtoto wa chekechea, niweke maandishi mareeeeefu

Soma vizuri MTAJI WANGU NI LAKI 6, ILA MAUZO YAKE HAYAWEZI FIKIA MILIONI NNE KWA MWAKA ILI NIKADIRIWE KUA MLIPA KODI HALALI

JE? NITUMIE NJIA GANI KUKWEPA USUMBUFU WA WATENDAJI... KWASABABU SIJAFIKIA HICHO KIWANGO CHA MLIPA KODI... LAKINI KULINGANA NA TAMAA YA WATENDAJI, USUMBUFU HAUTOKOSEKANA,.. JE? NI NJIA IPI NITUMIE ILI KUKWEPA USUMBUFU HUO

Ndugu kama bado huelewi, mmmhh basi niache na uzoba wangu, ila kama umeelewa ruksa kunishari
 
Lipa kodi halali utafanya biashara huru
Kwani sheria za ulipaji kodi zinaaza na kiwango gani stahiki ili uwe mlipa kodi halali?? Ninavyojua ni milioni 4, sasa mimi nipo chini ya milioni nne, nalipaje kodi ya hio biashara, labda kuwepo na mabadiliko kwamba kiwango chochote tunapaswa kulipa kodi
 
Njia pekee itakayomfanya asitengeneze 4m Kama faida ni kuuza mzigo kwa bei ya hasara hapo atakwepa kodi
Kuna mitaji ambayo hata uuze kiwango gani, huezi fikia mauzo ya milioni nne kwa mwaka, ila kama hata mtaji wa laki sita unaweza lipa kodi, sawa naweza wenda kuwa mlipakodi halali mana sitaki usumbufu
 
Mtaji lk6 mauzo 4m ndani ya mda mfupi utakua done kiongozi. Ukitoa mtaji hapo na ushuru na nauli unabaki na 3m c haba ukileta mzigo wa 3m faida 15m patamu usitusau kiongozi.
Jamaa kaongea kama kweli yani kirahisiiiiiii, hizi kejeli broo
 
Ukitengeneza ofisi ikawa kali sana lazima TRA wakufuatilie ila ukijibana bana kwenye mabanda hakuna wa kukufuata
Kidogo nimekuelewa, ila lengo langu sio kukwepa kodi, ila sijafikia kiwango stahiki cha mlipakodi
 
Kodi una-declare wewe. Mtendaji ni madra sana kuja kwako. Nenda TRA waambie makadirio yako. Inaitwa self-assessment for a reason.
 
Hao ambao hawajaelewa hawana uwezo wa kushauri chochote hapa. Yani mtu unashindwa kuelewa sentensi za kitoto namna hii sasa utaelewa nini maishani.
Ana mtaji wa laki 6, anatarajia kufanya mauzo ambayo ni chini ya milioni 4 kisheria ambayo ndio subjected to tax. Kama angekuwa anafika milioni 4 ndio alitakiwa akatwe kodi ila sasa hajafika hapo, je afuate utaratibu gani ili asilipishwe kodi na viongozi wa chini ambao ndio hulazimisha kulipisha kodi bila kuzingatia sana sheria.

Maelezo utapewa na wazoefu wa biashara ndogo. Na huu sio ukwepaji kodi kama wanavyosema, sio kila kibiashara chochote hata kuuza maembe ukalipishwa kodi. Ushuru, manispaa, usafi itategemea na halmashauri husika
 
Nyinyi ndio watu pekee ambao mna uelewa mzuri, yaani ulichozungumza ndicho nilicho maanisha mkuu... Hongera sana kwa uwelewa wako mkubwa... Nashukuru sana,.. Nina uhakika kama ungelikua una uelewa na hizo biashara. Nadhani ningefunga huu uzi... Shukrani sana broo

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Wanapozungumzia 4M kwa mwaka hawamaanishi mtaji ni kiasi gani wala faida ni kiasi gani wanaangalia total sales yako kwa mwaka ni kiasi gani.

Ngoja nikupe mfano.

Ikiwa mauzo ya nguo zako kwa siku pasipo kuangalia faida ni TSH 10,000 tu tafsiri yake mauzo yako kwa mwaka mzima yatakua ni 10,000 x 365 = 3,650,000/=
Hapo mauzo yako yatakua ni chini ya 4M kwa mwaka hivyo basi utakua exempted na kodi unachotakiwa kufanya ni kwenda Halmashauri kwa afisa biashara kisha TRA ukafyatue kitambulisho cha ujasilia mali kwa gharama ya TSH 20,000/=

Ikiwa mauzo yako kwa siku ni kuanzia 11,000/= na zaidi tafsiri yake kwa mwaka mauzo yako ni zaidi ya TSH 4,015,000/= hapa nenda TRA ukaombe TIN ya biashara ufanyiwe makadirio ya kodi na kupata tax clearance na uende Halmashauri kupewa leseni ya biashara.


Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Just do business don't bother with these constants... they are always there whether you like it or not...
Wasiwasi ndio akili mkuu, kuna rafiki yangu anaishi Tanzania na Kenya, last wiki alitoka Nairobi tukakutana somewhere katika mazungumzo yetu alinishauri na kunishawishi ni join the chain kwenye biashara ya mahindi ana network nzuri Kenya tutapiga pesa Mingu na ndio siri ya ukwasi wake, ni kweli ana pesa mingi Sasa hivi.

Sasa imagine Mimi ningekurupuka nainvest million 50 mzigo haujafika border vibali vya kuexport mahindi vimefutwa na serikali, hapo kifuatacho ni nini? Kwenda kwenye huduma ya Mwamposa au Mzee wa upako?
 
Hahahahahahahahaha kweli kaka wasiwasi ndio akili mkuu
 
Mpaka hapo kaka umenipa ufumbuzi mzuri sana.... Nashukuru sana mkuu ubarikiwe... Alafu Samahani mkuu,.. Hicho kitambulisho usemacho cha 20,000, sio hivi vya wamachinga, au ndio chenyewe
 
Yah kwa case hiyo ni sawa mkuu sababu ni biashara ya ku cross border, ila kwa case ya huyu mtoa mada mi naona kwa sababu atakuwa anachuuza tu kwenye soko la ndani haya mambaya TRA sijui nini asiyafikirie kwanza.. yeye apige mzigo kwanza, ukishaanza kuingiza pesa mbinu za kukwepa kodi utazijua tu... ila usianze kuogopa kabla hata hujaingia kwenye game
 
Nimekupata brother, point Nzuri ya kuishi nayo hii, thank sana broo
 
Mpaka hapo kaka umenipa ufumbuzi mzuri sana.... Nashukuru sana mkuu ubarikiwe... Alafu Samahani mkuu,.. Hicho kitambulisho usemacho cha 20,000, sio hivi vya wamachinga, au ndio chenyewe
Ndio hicho cha machinga. Wajasiliamali wadogo wote wanaitwa Wamachinga kwa jina la ujumla

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…