Biashara ya mtumba, mtaji laki sita, (mauzo chini 4m). Nifanyeje kuepuka usumbufu wa watendaji?


Band 1: Mauzo ambayo hayazidi Tshs4,000,000/= kwa Mwaka Hayatozwi Kodi(NIL)
Band 2: Ikiwa mauzo ni kati ya Tshs. 4,000,000/= and Tshs 7,000,000/= kwa Mwaka Kodi ni Tshs 100,000/
Band3: Ikiwa mauzo ni kati ya Tshs 7,000,000/= and Tshs 11,000,0000/= kwa Mwaka Kodi yake ni Tshs 250,000/=
Band 4: Ikiwa mauzo ni kati ya Tshs11,000,000/=andTshs 14,000,000/= kwa Mwaka basi kodi yake ni Tshs 450,000/
Band 5: Ikiwa mauzo ni kati ya Tshs14,000,000/=and Tshs 100,000,000/=basi Kodi yake ni Tshs 450,000/=

As per section 35 of TAA, Cap 438
taarifa hizo ni kwa mwaka 2020/21
 
Umeenda vzr san mkuu, bt kwenye kipengele cha kile kitambulisho cha mjasiriamali kwenye huu uongozi wa mama hakitumiki tena.
 
Duuuuu, safi sana Brother, umenifungua macho,.. Sasa kama kodi kwa mwaka mzima ni 100,000/=, kuna haja gani ya kukwepa?... Mi nadhani kuna changamoto ambayo mtu akijisajiri huko, inakua tabu zaidi.. Mana Kodi ya Tsh 100,000 kwa mwaka, ni pesa ndogo sana ambayo haiwezi kumfanya mtu afanye biashara kwa kukimbizana... Itakua kuna kasumba hapa katikati ambayo ukijisajili, inakua tofauti na utaratibu.. Tuweke wazi broo, vipi kuhusu hilo... Mana kwa kodi hio ya laki moja kwa mwaka,. Hata mchoma mahindi anaiweza kuilipa.. Labda iwe kwa mwezi ndio itakua changamoto
 
Ingekuwaw mimi ni wewe nisingehangaika na fremu kabisa

Kwenye fremu hasa mjini kuna mateso [emoji119]

Fanyia mezani Unachana Ballo unatafuta wale wa kupo into wanadaka mali , zinazobaki utaamua uuzie mezani au ukatembeze

Kwenye fremu hiyo analysis ya 4M ni kipengele labda fremu iwe ya chini ya 50,000 kwa mwezi ndo TRA watakuelewa
 
Ngoja nikusaidie nenda jiji omba fomu ya leseni nafikir hiyo biashara ni A watakupa utalipia kati ya 71k hadi 81k jaza kisha peleka ofisi za TRA ili wakupe TIN na Tax Clearance
Chief usiiogope leseni hata kidogo unachotakiwa kuogopa ni kodi za pango ambazo ndio kero kubwa kwenye biashara zenu!!
 
Sasa hapo si ndio itakuja ishu za kodi na mashine au inakuaje
 
Sasa hapo si ndio itakuja ishu za kodi na mashine au inakuaje
Mashine za EFD hautaulizwa wewe maana huna maingizio zaid ya mil 15 kwa mwaka uzuri serikali imeweka mazingira wezeshi kwako kufanya biashara we ukienda kukadiriwa ukiulizwa wastani wa mauzo kwa siku jibu ni kati ya 20k had 30k sasa kama utauza hadi 35k au 40k in actual market ni wew but mapato tayar unakuwa unalipa na utakadiriwa fairly tu.. Go ahead dont wait for the rocket science to shoot your business!!
 
Poa Brother nashukuru kwa ushauri wako, nitahakikisha naufanyia kazi kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…