Biashara ya nafaka

Biashara ya nafaka

Smith Rowe

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
4,319
Reaction score
9,003
Salamu
Tukumbuke kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni

Moja kwa moja kwenye mada
Baada ya kujichanga changa nimefanikiwa kupata ki 1M nataka kuwekeza kwenye nafaka (corona ikipoa) kama mchele na unga lakini swala ni kwamba bado nalifanyia tafiti soko lake

Nategemea baada ya kumaliza kidato cha sita (kama tutarudi shule) nitakuwa na kama 1.5M wakuu msaada wenu kidogo wa mawazo

Niwekeze kwenye bidhaa moja tuu au kotekote ?
Niifanyie mkoa gani mzuri?
Niwe na label yangu mwenyewe au mtaji hautatosha?
Nisimame mwenyewe au niwe na partner?
Nina mpango wa kufanyia hii biashara arusha japo sijawahi kuishi hii imekaaje?

Nategemea siku moja niwe na kiwanda cha nafaka. Ushauri wako ni wa muhimu sana
Nawasilisha....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom