Biashara ya nazi bei ya jumla

Biashara ya nazi bei ya jumla

Habarini wana jf......naomb msaada mwenye kujua kuhusu biashara hii anipe abc nina mtaji wa laki nne natak niagize nazi niiuze bei ya jumla kwenye masoko mfn. Ilala, temeke au bugurun
Ongeza pesa mkuu maana kwa mtaji huo labda ukawe mchuuzi kwny hayo masoko then ukauze kitaa, ila kwa kufuata shamba sio kweli, mi nimewahi kufanya iyo kitu najua abc zake
 
Habarini wana jf......naomb msaada mwenye kujua kuhusu biashara hii anipe abc nina mtaji wa laki nne natak niagize nazi niiuze bei ya jumla kwenye masoko mfn. Ilala, temeke au bugurun
Hili ndo tatizo la watu wengi wanapotaka kuanzisha biashara fulani, uanza kwa kujifungia ndani huku wakitaka wapewe ushauri!

Ww mwenyewe ndo inatakiwa ujitoe kwa Kufatilia huku na huko ili ujue utanufaika vp. Maana kama unayajua masoko kama hayo uliyosema hapo juu unashindwa vp kufika na kujionea mwenyewe mambo yalivyo.

Kwa upande mwengine unataka watu wakupe ushauri mbaya ili ushindwe kufanya kazi hiyo maana kama umedhamiria kufanya hilo lazima ujitoe mwenyewe.
 
Kama unataka kuuza nazi jumla kwa mtaji ulionao ushauri wangu:-

Tafuta wateja mmoja mmoja uwauzie jumla, sawasawa iwe kwa wauzaji wa nazi rejareja katika masoko makubwa au kusambaza kwenye magenge mitaani, ukipata wateja hata 3 au 4 wa uhakika, wanatosha kabisa kwa kuanzia.

Na wala usihofu kuuliza wauza magenge, maana hili ni jambo linafahamika, ukienda tu ukieleza kuwa unataka kuleta nazi unatafuta oda utapokelewa vizuri sana, maana kuna wauza magenge hawachukulii nazi masokoni bali wananunua kwa wauzaji wa jumla kama hivi.

Nb: Mara nyingi uuzaji wa namna hii unakuwa wa mali kauli.

Mbagala pale wapo wauzaji wa nazi rejareja ambao wanapokea mzigo wa hata nazi 2000 na pesa yako unaipata within 3 days

Sema tu kama iliyovyo jambo lolote halikosi changamoto basi na hii biashara inachangamoto, na moja ya changamoto kubwa ni madalali ndio maana sikushauri kupeleka mzigo sokoni.

Maelezo yangu hayajamaliza kila kitu ila yanaweza kukupa mwanga kidogo
 
Habarini wanaJF, naomba msaada mwenye kujua kuhusu biashara hii anipe abc. Nina mtaji wa laki nne nataka niagize nazi niiuze bei ya jumla kwenye masoko mfn. Ilala, Temeke au BugurunI
Nina mzigo wa nazi 200 nimevuna, naziuza zote kwa bei ya jumla, Kama upo serious njoo tufanye biashara.
 
Back
Top Bottom