Kama unataka kuuza nazi jumla kwa mtaji ulionao ushauri wangu:-
Tafuta wateja mmoja mmoja uwauzie jumla, sawasawa iwe kwa wauzaji wa nazi rejareja katika masoko makubwa au kusambaza kwenye magenge mitaani, ukipata wateja hata 3 au 4 wa uhakika, wanatosha kabisa kwa kuanzia.
Na wala usihofu kuuliza wauza magenge, maana hili ni jambo linafahamika, ukienda tu ukieleza kuwa unataka kuleta nazi unatafuta oda utapokelewa vizuri sana, maana kuna wauza magenge hawachukulii nazi masokoni bali wananunua kwa wauzaji wa jumla kama hivi.
Nb: Mara nyingi uuzaji wa namna hii unakuwa wa mali kauli.
Mbagala pale wapo wauzaji wa nazi rejareja ambao wanapokea mzigo wa hata nazi 2000 na pesa yako unaipata within 3 days
Sema tu kama iliyovyo jambo lolote halikosi changamoto basi na hii biashara inachangamoto, na moja ya changamoto kubwa ni madalali ndio maana sikushauri kupeleka mzigo sokoni.
Maelezo yangu hayajamaliza kila kitu ila yanaweza kukupa mwanga kidogo