Biashara ya ndizi na parachichi toka Tarime kwenda Mwanza

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Juzi nilikuwa nimeenda kule Tarime nimekutana na fursa nzuri sana kwa vijana walio serious, kule ndizi ni bei rahisi sana na parachichi hazina mnunuzi zinaozea shambani.

Kama una mtaji wa shilingi laki 5 unaweza kuifanya biashara hii ya ndizi na parachichi ukapata mafanikio makubwa, mfano Tarime mkungu wa ndizi wenye ndizi 80~100 unauzwa shilingi 6000~10000 ili hali kwa Mwanza ndizi moja inauzwa 200~300,

sasa biashara hii utaifanya hivi ukishanunua ndizi wako toka Tarime ukawasafirisha mpaka Mwanza utawavundika wakiiva unawasambaza kwa wauzaji wa reja reja, mamantilie na mahoteli nina uhakika kwa mtu aliye serious biashara hii itamlipa kwa muda mfupi sana.
Vijana mliopo kanda ya Ziwa changamkia fursa.
 
Umetembelea kwenye mawazo yangu mkuu, nimewaza hiki kitu muda mrefu nikimaliza masomo nitakifanya.
Fursa adhimu sana kwa siku unaweza kuingiza mpaka elfu faida na husumbuani na TRA.
 
Zile ndizi zikiisha iva hazimalizi siku hazijaoza mkuu,hii biashara watu walisha ijaribu wakaona ni hasara
 
Ukifata taarime kwa bei hiyo utakutana na changamoto kubwa ya soko kwa madalali hapa Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…