Biashara ya nguo mnadani

Biashara ya nguo mnadani

Mdau tu

Member
Joined
Jun 8, 2024
Posts
22
Reaction score
22
Habari zenu wadau naimani mungu Bado anatueka salama
Leo nimekuja naombeni ushauri kuhusu biashara ya kuuza nguo minadani Kwa kufungua baloo kabisa je itanilipa nimepanga kumuajiri mtu awe anatembea na mnadani Ani Kwa wiki aweze kwenda minada ata mi4 je hii itanilipa wadau tupo apa kusaidiana mawazo naomba msaada Kwa hilo
 
Ndio inalipa. Wewe umepanga kuianzishia wapi?
Mchawi ni location na target market ya watu unao walenga. Maana kuna mabalo ya nguo za watoto nguo za wanawake na wanaume, wewe umepanga kuuza aina gani ya balo?

Ukipata minada iliochangamka basi mzigo utaenda.
 
Minadani wanauza vitu cheap.wanataka vitu vya bei Chee..nguo za bukubuku ndo kwao.kama unapeleka nguo za gharama hapana pia huyo unaemwajiri anaweza kukuibia.
 
Nataka niwe nafungua balo za nguo zozote nahesabi idadi ya pic zilizopo then namgei uyo mtu akauze na kuhusu mnada nataka uwe mnada wa kutembea maan kuna wanaotembea na minada unakuta kwenye wiki mtu kaenda ata minada mi4
 
Nataka niwe nafungua balo za nguo zozote nahesabi idadi ya pic zilizopo then namgei uyo mtu akauze na kuhusu mnada nataka uwe mnada wa kutembea maan kuna wanaotembea na minada unakuta kwenye wiki mtu kaenda ata minada mi4
Hapo pesa ipo.
Shida ni kupata sypplier mzuri wa mabalo
Ukisha fungua balo tumia stratehy hii. una grade hivi
1 nguo nzuri ziuzwe kwa bei nono kidogo kias kwamba ina rudisha pesa ya mzigo au robo tatu yake
2 nguo zilizo za wastani yaan hazijachakaa wala si mpya uziuze kwa bei itakayo cover nguo zilizo chakaa au maronya
3 nguo zilizo chakaa= uza bei ya kwaida ndo hzo unaskia ata kwa buku.
Biashara hii inaendana na msimu. Hakikisha pesa ya mzigo/ balo inarudi na kuongeza faida
 
Back
Top Bottom