Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mahitaji ya nyumba ya kulala wageni yapo kila sehemu hasa kama kuna shughuli za uchumi mfano mgodi wa madini, kilimo hasa cha mazao ya biashara kama pamba na korosho.
Hata shughuli za utalii zinaleta fursa kwa nyumba za wageni hasa kwa wale low budget tourist. Siku hizi Waafrika wanapenda kutembeza watoto katika nchi zenye vivutio. Unaweza kukuta familia ina budget ya $500.
Mwenyewe uwe na mapenzi na biashara hii. Uwe na uzoefu kidogo na housekeeping, catering na bar tender.
Kwa nyumba ya vyumba 20 kuwa na kama shuka 200. Si lazima ufue kila siku unaweza kufua mara mbili kwa wiki kama ni low season.
Uwe na washing machine hata ya kilo kumi inatosha. Shuka zinazochafuka sana tupa zitakugharimu kuzirudisha katika ubora.
Uwe na uhakika wa maji na umeme.
Usiku mmoja Tshs 5,000, kifungua kinywa kinaweza kuwa ndizi, matango, chai au kahawa, mayai mawili na kipande cha mkate.
Kwa anaetaka kula mchana, atoe order wakati wa chai na wa usiku waeleze mapema.