Biashara ya Petrol Station

PARADIGM

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2014
Posts
2,774
Reaction score
1,827
Habari za majukumu wadau. Nina wazo la kuanzisha biashara ya petrol station lakini sina uzoefu wa biashara hii. Linalonifanya kuwazia aina hii ya biashara ni kwamba nina site Dar ambayo nafikiri ni potential kwa hii biashara. Nina eneo la 3000 square meter na hivi karibuni barabara inayopita site imefanywa kuwa barabara kuu na tayari imepigwa lami.

Naomba kujua yafuatayo:

1) Vibari vinavyotakiwa ili kuanza hii biashara, mamlaka zinazotoa vibari na gharama za vibari.

2) Investment cost za kujenga visima na kununua mashine za kupump.

3) Margin ambayo mfanyabiashara anapata kutokana na bei elekezi ya Ewura.

4) Operating costs unazotakiwa kuzi meet. kwa mfano wafanyakazi wa petr

5) Changamoto za biashara hii

6) Pia niliwahi kusikia kama una petrol station facility unaweza kupata mali (petrol) kwa credit kutoka kwa suppliers wa mafuta. ni kweli hili?

Nitashukuru kwa ushauri wenu.
 
Mtaji wake ni mkubwa, ila kama hela ipo hakishindikani kitu, ila ngoja wataalam waje waelezee kiundani zaidi wote tupate kufahamu
 
Mtaji wake ni mkubwa, ila kama hela ipo hakishindikani kitu, ila ngoja wataalam waje waelezee kiundani zaidi wote tupate kufahamu

Hajataja budget yake, anahitaji kujua tu gharama na taratibu.
 
Mkuu sina uzoefu ila ukiwa na wazo la kuingia ubia kwenye hilo eneo tuwasiliane pm.
 
Mtaji wake ni mkubwa, ila kama hela ipo hakishindikani kitu, ila ngoja wataalam waje waelezee kiundani zaidi wote tupate kufahamu

Hili wazo la biashara liko kwenye infancy stage. Ndiyo maana najaribu kukusanya taarifa za msingi ili niweze kuwa informed na baadae kufanya decision. Hata kama mtaji ni mkubwa nafikiri halitakuwa tatizo kama biashara inalipa.
 
Mkuu sina uzoefu ila ukiwa na wazo la kuingia ubia kwenye hilo eneo tuwasiliane pm.

Ahsante mkuu. Ila kama ubia sijui ABCD ya biashara hata negotiation ni ngumu. Hata hivyo ni wazo zuri kwani hiyo ni plan B baada ya kufanya analysis nikaona kama nitaweza au la? Kama sitaweza nitakuja kwenye hiyo option.
 
Hili wazo la biashara liko kwenye infancy stage. Ndiyo maana najaribu kukusanya taarifa za msingi ili niweze kuwa informed na baadae kufanya decision. Hata kama mtaji ni mkubwa nafikiri halitakuwa tatizo kama biashara inalipa.

Mafuta yana lipa mkuu...sawa nimekupata chief
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…