Jamani nimetumbukiza mguu kwenye hii biashara ya Pharmacy. Nimeanza kuonja joto ya jiwe, hasa kwenye upatikanaji wa pharmacists na ushindani wa maduka ya dawa baridi ambayo hayana vibali lakini mengi yanauza dawa aina zote.
Naomba msaada kwa wenye uzoefu, pharmacists, nawapataje na kwa bei gani kwa sasa?
Je, kuna umoja wowote wa wenye biashara za pharmacy?
Na challenge nyinginezo ambazo bado nitaendelea kukumbana nazo naomba mnijuze.