Biashara ya Rice Combined Harvester v/s Mashine ya Kukobolea Mpunga

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Habari za Wikiend Wadau,

natumai mko poa, nafikiria nijihusishe na Biashara ya Mpunga, lakini sio katika kununua au kuuza mpunga wenyewe, bali kuvuna au kukoboa mpunga wa watu wengine. Yaani ninunue Rice Combined Harvester au Mashine ya Kukobolea Mpunga kisha niiweke mahali, watu wakija kuhitaji huduma wanalipia.

Sasa msaada wangu naouhitaji kutoka kwenu wataalamu wa hii biashara ni ufuatao,
1) Ni biashara gani katika hizi mbili inalipa zaidi (i.e Harvester au mashine ya Kukobolea) na yenye "payback period" fupi au ya mapema kuliko ingine?
2) Wapi nitapata mashine za hiyo inayolipa (Either Harvester au mashine ya Kukobolea) kwa gharama nafuu zaidi,
3) Ni aina gani ya mashine ni nafuu na durable zaidi kwa shughuli hizi za zinazohusisha uvunaji mkubwa zaidi?
4) Ni maeneo gani au mashamba yepi nikipeleka hizi mashine basi wateja ni wengi hivyo uhakika wa mashine kufanya kazi ni mkubwa?
5) Maoni/Ushauri mwingine wowote unakaribishwa

Karibuni
 
Fanya feasibility study ya
1)Wapi Mpunga Unazalishwa Sana
2)Kwa sasa Uvunaji unatumia technology ipi--Mfano Shinyanga hadi Morogoro wanatumia manual,kwani ni small scale,Mbeya wako mechanised hadi Kuvuna
3)Wakati usio wa mavuno machine zinafanya nini?
In this case machine ya Kulipia inamake sense,kwa kuzingatia Wakulima wetu wengine ni small scale.
 
Mku wangu ndio maana nikalileta hapa jamvini tusaidiane mawazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…