Biashara ya Soft Drinks

Biashara ya Soft Drinks

monta

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2014
Posts
1,271
Reaction score
1,803
Wakuu nimekuwa nikipambana kila leo kufikiria natoka vipi ilhali elimu yetu bongo haina msaada wowote(tunakaa na vyeti ndani). Kuna biashara nilikuwa nafanya mkoa fulani kwa takribani miezi 6 toka January na ilikua inanilipa 10k per day, almost 300k per month. Wiki mbili zilizopita imepata changamoto toka utawala wa sasa na kupelekea kuflop (nimeifunga).

Nimekuja na plan B ya kuanzisha biashara ya Soft Drinks nikiwa nimefanya research kiasi fulani. Nataka nitafute freezer (BOSS) litre100 na dell 2 za kuanzia kwa ajili ya kusambaza ice cream mashuleni na vinywaji baridi kwenye fremu niliyokuwa nafanyia biashara ya awali.

Nitakuwa nauza Soda, Maji, Juice, Maziwa, Ice Cream na Barafu. Je, kipi niongeze au nipunguze katika biashara hii? Na changamoto zake hasa na zipi? Faida nayo inakaaje? Vipi kuhusu TRA nao wanasumbua au kitambulisho cha mjasiriamali kinatosha.

Ahsanteni.
 
Congrats, kama ulifanya research basi kuna changamoto ulizigundua anza biashara haraka iwezekanavyo mengine yataijirekebisha kadri utakavyoendelea kufanya utajua mahitaji ya biashara yako.
 
Congrats,kama ulifanya research basi kuna changamoto ulizigundua anza biashara haraka iwezekanavyo mengine yataijirekebisha kadri utakavyoendelea kufanya utajua maitaji ya biashara yako.
Shukrani mkuu nashukuru kwa ushauri.
 
Hali ya hewa ndio changamoto kingine labda umeme! Kila penye nia pana njia! Kila LA kheri
 
Hali ya hewa ndio changamoto kingine labda umeme! Kila penye nia pana njia! Kila LA kheri
Shukrani mkuu, umeme niliweka mita yangu kwenye biashara ya awali kwahiyo nitatumia hiyo, hali ya hewa nilipanga niwe na biashara ya ziada ikifika kipindi cha masika maana joto lipo nyakati zote za mwaka.
 
Shukrani mkuu,umeme niliweka mita yangu kwenye biashara ya awali kwahiyo nitatumia hiyo,hali ya hewa nilipanga niwe na biashara ya ziada ikifika kipindi cha masika maana joto lipo nyakati zote za mwaka
Vizuri! Hata hivyo biashara karibia nyingi kuna msimu zinafifia kidogo! Nadhani utakuwa muda wa mapumziko kwako[emoji12]
 
Back
Top Bottom