OGOPASANA
JF-Expert Member
- Apr 30, 2009
- 262
- 144
Heshima mbele wakuu, nimekuwa na wazo kuhusu jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana hapa nchini kwetu katika nyanja za biashara hasa kuhusu kufanya biashara kama wabia, yaani vijana kama 50 ambao wataaminiana, kufahamiana vizuri na kuwa na vision moja na kuanzisha kampuni kuendesha biashara yoyote watakayokubaliana kwa kuchangia mtaji wa walau Milioni 2 kila mmoja ambapo kwa watu 50 wataweza kupata mtaji wa Milioni 100 ambayo nahisi ni kiasi tosha kuanza kuanzisha kampuni ndogo endelevu kisha wao wakawa shareholders na hapo hapo wakaweza kujipatia ajira. Kwa wenye uzoefu, hili lina ugumu gani, hasara gani, faida gani hapa nchini?