Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Short white

Senior Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
124
Reaction score
32


Salaams JF,

Nilipata wazo la kuanzisha bakery maeneo ya Sinza. Products ni ; Mikate, Maandazi na cakes aina mbalimbali. Sikuomba au kutafuta ushauri kwa mtu yeyote. Pia sijafanya research ya uhakika kuhusu mahitaji halisi ya hizo bidhaa ninazotaka kuingiza sokoni. Pia sijafanya utafiti kuhusu ushindani wa hii biashara. Nimeamua kuchukua RISK 100% katika kuwekeza huko kwenye bakery. Kwahiyo bado sijaelewa / sijajua kama nipo njia sahihi au nimekosea. Naomba ushauri na uelewa wenu kwenu hii biashara.

Hadi sasa nimefanikiwa kupata vitu vifuatavyo;
- Machines- 3 Ovens ( moja kubwa inaingiza paltes 6 na nyingine mbili ni ndogo zinaingiza plates 2 kila moja); 1 Mixer aina ya B30; Shelf; 30 Oven Plates,
-Nimepanga Jengo na kulifanyia ukarabati kulingana na mahitaji ya kazi.
-Nimesajili jina la biashara
-Nimeshapata na TIN
-Nimeshapata leseni

Vitu vinavyohitajika kwa sasa ni;
-Connecting service line ( electricity) kwenye jengo ambalo nimeshafanya wiring
-TFDA authorization
-Source of more finance
-Hard working, knowledgeable and skilled person ( Baker) ambaye ataweza kutengeneza bidhaa mbalimbali
-Bread slicer
-Manager and cashier
-Marketing and sales person
-Distributor

Je mnaonaje wakuu? Je nipo sahihi? Nawakilisha

WADAU WENGINE WANAOHITAJI UFAHAMU WA BIASHARA HII


MICHANGO YA WADAU
 
Kuna ndugu ameniomba ushauri wa kununua vifaa vya bakery.

Naomba maelekezo ya vifaa umenunua wapi? Ni hapa nchini au umeagiza nje na je ni brand gani?

Usiwe na wasiwasi mkuu, pengine mimi ni mshindani, la hasha, hata hivyo Dar ni kubwa, kwenye soko kila mtu ana riziki yake.
 
Hongera sana! sasa kaza mwendo kuifanya kazi kwa bidii zote,utafanikiwa tu ,usihofu wala haihitaji others approval.Mungu awe nawe.tupe jina la hiyo sehemu,tuwe wateja.
 

Newazz, vifaa vya bakery vinapatikana city center opposite na JMO building kwenye duka la BAJERYA. Bajerya ni brand name ya hizo vifaa. Ahsante kwa comments zako.
 
hongera sana! sasa kaza mwendo kuifanya kazi kwa bidii zote,utafanikiwa tu ,usihofu wala haihitaji others approval.Mungu awe nawe.tupe jina la hiyo sehemu,tuwe wateja.

Mutisya Mutambu, nashukuru sana kwa ushauri wako na baraka zako. Nitazifanyia kazi.

Ahsante
 
hongera sana! sasa kaza mwendo kuifanya kazi kwa bidii zote,utafanikiwa tu ,usihofu wala haihitaji others approval.Mungu awe nawe.tupe jina la hiyo sehemu,tuwe wateja.

Mutisya Mutambu, nashukuru sana kwa ushauri wako na baraka zako. Nitazifanyia kazi. Ahsante
 
Hongera sana kwa udhubutu wa kujaribu kufanya,,usiangalie kushindwa kamwe, kuwa na mtazamo chanya wa kushinda maana yote yanawezekana, jipange vizuri, angalia wengine walio kwenye hiyo biashara wanafanyaje na ujifunze kwao, buni njia binafsi za ushindani ili uweze kupenya kwenye soko na kushindana na nao, mtangulize MUNGU akupe busara, hekima, maarifa na nguvu ya kuendelea kufanya (persistence) hata utakapofikia pagumu, (put in mind that good idea, good plans, hardworking, perseverance and persistence will make you at the top of the ladder)
 
Hongera kaka kwa kudhubutu,kwani ni wachache wanaoweza kufanya hvyo.

Ushauri: jitahdi kutangaza biashara yako, pia tafuta masoko kwenye maduka madogo madogo na makubwa,kwani kuna kuwa na ugumu kuingza bidhaa mpya sokoni kwasababu maduka takribani yote yanatayari mali inayofanana ya zako, kwahyo pitia ktk maduka kwa kuchunguza wanauziwaje bidhaa kama yako ili wewe uweze kupunguza kidogo ili bidhaa yako iweze kuingia sokoni.

Then ujitahdi kutengeneza kitu cha tofauti na unaowakuta sokoni.

Ntarudi tena baadae.
 

Huu ushauri ni wa great thinker. Naomba uuzingatie sana utafanikiwa
 
Short White hongera sana kwa kuamua kuwa mjasiriamali.

Bidii na kutokata tamaa ndiyo kitu cha msingi changamoto kwako zifanye mlango wa kupata fursa pia.

Ukiangalia bidhaa nyingi sana za kutoka Bakery, ikiwemo mikate, skonsi, keki na vinginevyo bado havijamlenga mtu wa kipato cha chini unaweza kubuni jinsi yakuwafikia hao ikiwa na pamoja kutengeza bidhaa watakazomudu, ikiwa ni kufungasha kwa kiasi fulani. Mfano mfuko wa skonsi unakuwa na skonsi kumi unaweza kufanya nusu yake, sina uhakika na eneo ulilopo lakini hapo ulipo unaweza pia kuuza bidhaa zako kwa kufungua duka, ikiwa na pamoja watu kupata mikate, skonsi fresh.

Chunguza ladha ya bidhaa nyingine za kutoka Bakery na watu wanapenda ladha ipi,kwani kuna watu wamepotea kwenye biashara hii kwa kuharibu ladha la bidhaa zao.

Huu ni mtazamo wangu,nakutakia kila la kheri katika kufanikisha ndoto zako.
 
You are already a business personality. Why going back, wanna be 'poor dad'?
 
Hongera kwa Kuthubutu.

kupata baker mzuri siyo jambo rahisi,ila inawezekana kumuiba mmoja kutoka ktk bakery nyingine,hapo inabidi utembelee bakery nyingine ujue average ya mishahara ,then uanze zoezi la kupata a good baker.uichukue unemployed baker, tafuta aliyekazini umuamishe.

2.distribution nzuri ni via watu wa baiskeli/pikipiki.hapo ukifanikiwa kinachobaki ni smiles all the way to the bank
 
Good Trial Mzee, Nadhani ni mwazo mzuri sana na kikubwa hapa ni ninavyoona Jf ilivyo msaada kwa kila kitu, kwa kweli hii ni home of Great Thinker hakuna kitu una-initiate then usipate walau Mchango wa mawazo utakaosaidia kwa namna moja ama nyingine.

My contribution:

Fanya Utafiti wa namna unavyoweza kuongeza uimara, Decorations na ubora wa packaging Material.
Ukifanikiwa kupata Graphics designer mzuri akakusaidia ku-design ile mifuko mizuri kwa maana ya mwonekano na hata ilawa tofauti na hii iliyozoeleka Naamini itakuwa ni Moja ya bao utakalopiga.

Ili kuwa tofauti na washindani wako unaowakuta sokoni, unaweza kuwa unaweka hata Kiasi kidogo sana (Ujazo wa Kijiko Kimoja kikubwa cha chakula) Blue band ambazo pia unaweza kuwa umeagiza special Order kwa Watengenezaji ikiwa na Logo yako then kwenye hiyo packaging ya kate unaweka hiyo Blue band yenye logo yako.
 
Kuna jamaa anaitwa Thomas mikate, yeye yupo DAR, anuaza mikate mingi sana kwa kutwa,ni rafiki yangu kwa uteja kwake.

- Hana brand wala Duka la mikate yeye anauzia ktk gari lake,ni suzuki mini van,kadogo hivi rangi ya blue na pia anayo nyeusi,huwa anapaki station opposite TRA offices ,jioni na pia huwa anakuwa maeneo ya posta karibu na CRDB holland house or ifm area.

Mwaka 2009 aliniambia kuwa anapata daily profit ya 140,000. na kuwa mikate yake huwa haibaki.jaribu kumtafuta atakushauri ni mtu muelewa,ila hapendi watu wa TRA(kodi etc) walishawahi kumsumbua ndio maana hana BRAND ya mikate yake,

Inasadikika kuwa bakressa wa Azam huwa ananunua mikate yake kwa matumizi yake na wajukuu zake.
 
Ndugu wazo zuri, ila hapo kwenye red, kwanini kimoja usishike wewe kama ndio kwanza unatafuta more finance, hadi ujue ABCs ya biashara yako ndio unawaachia watu kila kitu la sivyo mmmmh
 
Umesahau kitu kimoja mkuu, sasa nikuchapa kazi kwa nguvu zote, high supervision bila kuleta mchezo especiallly kwa vijana wakowa kazi, pesa imeshatoka inatakiwa irudu na faida sinza ni good location, watu wa sinza hawapiki bwana utawapata tu. usisahahu na kuwawekea ka cafe kwa ajri ya chai.
 
Naomba ushauri,

Tuna kikundi chetu cha kina mama na tunataka kuanzisha project ya bakery, Please naomba ushauri ya makadirio ya gharama ya kuanzia,Kama inawezekana orodha ya vifaa vinavyoitajika ili kutuwezesha kuanza project yetu.

Natanguliza shukrani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…