Biashara ya Usafirishaji Abiria

Basham

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2014
Posts
743
Reaction score
434
Amani iwe kwenu wana JF

Kama heading ilivo

Naitamani sana hii Biashara ya usafirishaji wa abiria hasa hasa ya haice ndo ninapotaka kuanzia kabla sijaingia kwenye mabasi makubwa, Mwenye ujuzi nayo naomba anidokezee vipi inaendeshwa faida yake changamoto n.k
kuna kauli mbili kwenye hii biashara. Je, ni biashara pasua kichwa kweli kama wengi wanavodai au ni biashara ambayo inaweza kukufanya kua milionea ndani ya muda mfupi, hizi ni kauli zinazonipa utata sanaa...

Karibuni kwa mawazo yenu

Wasaalam
 
Mimi pia nimeingia bila kuielewa vizuri biashara hio hivyo tusubiri wenye uelewa mzury watufahamishe
 
Ipo vizuri cha msingi ni kukomaa na kuipa gari service nzuri..
 
Ipo vizuri cha msingi ni kukomaa na kuipa gari service nzuri..
Changamoto zake ni zipi, bus or haice gani ni nzuri na mtaji unahitajika kiasi gani n.k
 
Nasubiri muongozo wakuu kuhusu hii issue
 
Nakushauri, kwa kifupi tu. Tafuta biashara nyingine ufanye na sio ya daladala.
 
Nakushauri, kwa kifupi tu. Tafuta biashara nyingine ufanye na sio ya daladala.
asante mkuu kwa ushauri wako, lakini naomba unipe sababu in detail mkuu
 
Hii biashara ni ya uhakika pia ina uhakika wa kuleta faida katika muda mfupi kwa vile wateja wapo tele. Kimsingi unatakiwa ukaribu na ufuatiliaji ulio makini, mwanzoni usiwe mbali na wafanyakazi wako, hakikisha matengenezo ya kawaida yanafanyika kama vile kubadilisha oil kwa wakati. Hakuna kucheka na wafanyakazi wako, mahusiano siku za mwanzo yawe kama ya paka na panya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…