Biashara ya vifaa vya simu

sheby dunia

Member
Joined
Jul 12, 2018
Posts
78
Reaction score
83
Habari wakuu naomba ushauri, hivi eti kwa mtaji wa 450,000/= ninaweza anzisha biashara ya phone accessories vifaa vya simu.

Note: Hiyo 450000/= ni kwa aajili ya kununua bidhaa tu na sio marekebisho ya ofisi.
 
Unataka uuze covers?
Earphones?
chargers
Protectors
Batteries
LCDs
..Basi hiyo Ni pesa kidogo sana Ila nikijua location na walengwa wako/wateja nitakushauri.
 
Sijawahi fika Ila Kama wateja wako/walengwa Ni wapenda vitonga...wananchi wa Hali ya chini ..

Anza na earphones za buku Mia mbili kwa buku Mia 3 whole sale..
Covers Autofocus nyingi zinakuwa black in colour Bei 1000,1500 elfu mbili kwa whole sale..

Batteries za simu ndogo viswaswadu.. za buku buku jero whole sale..
Housings za simu..nokia.sana Sana..bse ndo zilizopo available .sokoni
Bei Ni buku Kwa housing Pekee ..na buku jero kwa housing yenye motherboard...

Kuongeza kipato na kuvutia wateja ..mtaji ukikuwa au Kama unaweza azima ..tafuta computer Tia nyimbo na sizoni...
Uza..

Pia usisahau kuuza memory cards flash disks..
Za kiwango Cha chini na Cha juu(Fake na original)
Karibu mkuu.
 
Poa kaka na vipi kuhusu faida
 
Poa kk na vp kuhusu faida
Faida inategemea na wewe unataka kwenye kila item sh ngapi...
Mfano unaponunua battery buku unauza buku 3..
Ya buku jero unauza buku 3..
Ila mzunguko wao utaamua.. uuze kwa faida ya Tsh ngapi..
 
Mkuu hiyo pesa ni kubwa sana na kama ukipata location nzuri faida inakuja kama huo mtaji wako.

Ila fanya kwanza utafiti wa wateja wako maana waweza weka vifaa ambavyo wateja wako hawavihitaji.

50 cent katika kitabu chake 50th law anasema "Start even if you are not ready". mtaji haujawahi tosha hata siku moja.
 
Poa kaka unapaikana mkoa gani?
 
Weka na ufund simu hapo unapofanya hayo mambo
Sitaki kuusikia huo ufund maana hapa yenyewe ni fundi PC ndomana nataka nifungue BIASHARA engine MNA ufundi stress Mara polisi yaani bora niwe mganga kuliko kuweka ufundi simu ndio maana natafuta BIASHARA engine itakua haina stress na lawama kama ufundi. Unapga laki Leo kesho unapasua kioo cha A20 unaenda kulipa polisi 170k. Full stress.
 
Mbona hatari
 
Ha ha ha unakuwa fundi unategemea pesa ya mteja lazima uwe na stress
 
Hongera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…