Biashara ya vinyago

Biashara ya vinyago

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
863
Reaction score
408
Jamani wadau,
Naomba kuuliza biashara ya vinyago kwa wale wenye ufahamu. Jinsi inavyofanyika na faida yake ilivyo. Nitashukuru
 
Mkuu hii biashara ilikuwa More Profitable zamani hizo, kabla Dunia haijawa kijiji, hivi sasa Watalii wengi wanao kuja Tanzania hawana haja ya Kununua Vinyago tena kwa sababau maduka ya huko kwao vimejaa tena cha ajabu vinauzwa bei ya Chini kuliko huku Tanzania,

Kwa sasa watu wana export sana Vinyago kwa njia za DHL na zingine kwenda kwenye Maduka ya vitu vay kitalii huko Ulaya na Marekani,

ila jaribu kuongea na wanao fanya hii biashara, watakupa more detail, na unaweza kufanya biashara ya vitu vingine vya asili kwani viko vingi tu
 
Tafuta Location Nzuri kama kwenye mahoteli ya Kisasa ambapo kuna watalii wa mara kwa mara.
Sea Cliff pako poa as maduka ya vinyago pale ni machache sana na kuna namba kubwa ya wageni maeneo yale. Ila rent yao ni kichapo kiaina (1480USD) kwa mwezi)
Slip Way ni mashuhuri sana kwa hii biashara, ila siku hizi wanataka uende na kitu "Unique" ili wakubali kukupa Frame.
Holiday In, Kilimanjaro Kempiski, Double Tree naona kama hapajachangamka sana kwa hizi dili (mtazamo wangu)
Maeneo ya Mitaani kama Mwenge n.k utatakiwa uwe shapu sana as utakutana na competition ya fellow wauzaji.
Na kama una ndugu ama marafiki nje ya nchi ongea nao wawe wanafanya Marketing kisha wewe unawatumia mzigo (hii inalipa sana kama huyo mtu akichangamka, japo utakumbana na baadhi ya vikwazo kwenye kusafirisha idadi kubwa ya Vyinyago)

Kila la Heri Mdau.
 
Ukitaka kujua kiundani nakushauri utembelee pale Mwenge, wataweza kukupa taarifa muhimu kuhusu upatikanaji wa mzigo. Wapo wafanyabiashara wanaosafiri kufuata mzigo wenyewe. Pia wapo wauzaji wa jumla ambao ukishajiingiza kwenye hii biashara na wakakuzoea wanaweza kukupa mzigo kwa mali kauli.
 
Ukitaka kujua kiundani nakushauri utembelee pale Mwenge, wataweza kukupa taarifa muhimu kuhusu upatikanaji wa mzigo. Wapo wafanyabiashara wanaosafiri kufuata mzigo wenyewe. Pia wapo wauzaji wa jumla ambao ukishajiingiza kwenye hii biashara na wakakuzoea wanaweza kukupa mzigo kwa mali kauli.
Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom