Cha kwanza kabisa ni kuchagua eneo /location ambao Kuna maduka madogo madogo , maeneo yenye gorossary nyingi, Kiujumla eneo liwe limechangamka, Faida kwenye vinywaji ni ndogo sana , kunahitajika update mzunguko mkubwa.
Bidhaa za kuwwka:-
Azam - Azam energy, Ember juice, apple punch, malt , coffee malt, ukwajuu, Swiss, fursana, cola, tangawazi. Maji ya Uhai size zote.
MOE- Moe Xtra, Maji yake, juice ndogo aina Pride , malt ya nanasi
Sayona:- Soda za tangawazi , sayona soda na Maji
Oilcom (watercom) ; Maji afya, energy zake na soda za afya
Pepsi Cola; soda zao zenye soko sana ni Pepsi hizi nyingine chukuwa kidogo na Sasa Wana Pepsi max inakimbiza sokoni.
Coca cola; soda zao zote karibu zinatoka sana
Coca cala nunuwa sana hizo ndogo za take away maana mtaji wake ni manunuzi hakuna creti Wala chupa, piya weka take away. Kubwa.
NB:- Tengeneza mikokoteni mitatu ya tairi za baiskeli ya kusambazia bidhaa Kwa wateja.
Hakikisha Cha kwanza Kila siku nikupigie simu wateja nakuwaulizia uwapelekie bidhaa sio ukae dukani usubiri wteja. Hakikisha unakwenda kutafuta wateja huko makwao. Sio unaka tu.
ANGALIZIO Faida Kwa soda ndogo na Maji madogo. Isizidi 200/250/= per cartoon. Soda kubwa take away na creti. Iwe 500/= mchawi wako nikuongeza maudho.
Nenda depot yoyote hizo company au piga simu toa order watakuletea mzigo Hadi ofsini kwako.
Mwanzoni chukuwa mzigo kidogo kidogo kujuwa eneo husika wanapenda product Gani? Ila kuna zile common kukimbiza ni kawaida mfano Azam energy, Moe Xtra inauza, na nyingine. Piya sio vibaya ukapita maduka yaliyojirana na eneo unalotaka kufungua ofisi Uwezi kuona bidhaa Gani wanaxzo Kwa wingi? Bei zao? Huduma zao zipojee? Eli wewe uanzie hapo.