Biashara ya vipodozi Vs Electronics

Beberu

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2017
Posts
4,548
Reaction score
9,740
Wakuu heshima yenu
Sasa ndugu zangu kijana wenu nina mtaji wa M5 nipo nafikiria kuanzisha biashara moja kati hizo 2 hapo ndani ya mji wa Dsm maeneo ya mbezi mwisho au kimara

Kwenye biashara ya vipodozi nisiwafiche nahofia ukweli kuwa mimi sina ule muonekano wa ki hb wa kusimama dukani (sijui ni mawazo yangu tu kuwa lazima muuza vipodozi au hb/cutie) hapa nataka kuuza
Perfumes
Spray
Mafuta
Deodorants
Hereni
Bangili
Saa

Biashara ya electronics hapa nataka kuuza
Switches
Bulbs
Wires
Pipes
Extensions and the likes

Sasa wakubwa zangu mliozoea biashara naomba mnisaidie mawazo yenu ni ipi biashara itakayonifaa zaidi na kwanini ?
Nb
Ndo naanza maisha kwa hio mimi ni mgeni katika biashara
Nafikiria pia kuweka mobile money katika hizo biashara kwa mtaji mwingine wa pembeni kama 1.5M hiv

Natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwa mchango wenu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Zote ni biashara zinazo trend sana , haswa vipodozi kwa vile wahusika wengi ni wanawake, kama ijulikanavyo wanawake asilimia kubwa bila urembo hawawezi kuishi.

Lakini kwa namna watu wengi wanavyo jenga na teknolojia ya ujenzi inavyo kua kila siku , biashara ya vifaa vya umeme ni bora zaidi.
 
Zote 2 inawezekana. Lakini kikubwa Location ya kuweza hizo biashara na pia elimu kidogo juu ya hizi Biashara inatakiwa! Pia Mtaji unaanza nao na yenyewe ina impact na hii Biashara
 
Tafuta location nzuri fungua duka la mahitaji ya nyumbani..... Tafuta location ambayo kama kutakua na duka kama lako basi hilo duka liwe halijajitosheleza mahitaji.....
Weka nafaka, weka mafuta na vitu vingine vidg vdg zingatia usafi kushinda duka la jirani ako,
weka na gas na Airtel money na mpesa
 
mkuu wa umuhm upate location yeny mzunguk mkubwa wa watu.

ila electronic ni nzuri japo mahitaji yake sio makubwa sana ktk jamii namaanisha km bulb mtu atakuj kununua baada ya bulb nyngn kuungua kwhy ita take time mteja wa leo kuja tena.

kwenye vipodozi nadhan ndo pazuri zaidi wanawake wanapenda sana kujiremba na hata ukitazam idadi yao ni kubwa kwhy ukipata sehem na bidhaa zako zikiwa bei chin utaauza sana .

changamoto vipodozi vina mda wake wa kuexpry tu
 
Mtoa mada ameomba ushauri Kati ya vipodozi na electronics wewe unaleta habari za nafaka mara airtel money una akili sawa sawa kweli

Nimekaa pale njoo unipige
 
Mtoa mada ameomba ushauri Kati ya vipodozi na electronics wewe unaleta habari za nafaka mara airtel money una akili sawa sawa kweli

Nimekaa pale njoo unipige
🀣🀣, jau kweli Nkuu
 
Tronic ni bab-kubwa,hata vipodozi, japo issue ya EXP date sometimes ni zaidi ya changamoto[emoji221]
 
Vifaa ulivyotaja ni vya umeme(Electrical).
Electronics ni vifaa vinavyotumia umeme(kwa lugha rahisi). Electrical ni vifaa vinavyoleta umeme.
Mifano;
Electronics ni radio na accessories, tv na accessories, simu na accessories,
Electrical ndio kama ulivyotaja, nyaya za umeme, bulb, taa, tubelight na accessories.
 
Inapendeza na kila la kheri... Ngoja waje kukupa muongozo...
 

Biashara ya vipodozi ni nzuri ikiwa unaanza lakin ikikua changamoto tbs watakusumbua
Ila kwa upande wa vifaa vya umeme ni more valuable sijajua ni mbez sehmu gani exactly
Ila kwa upande wa mbez mwisho fungua mgahawa wa wastani tafta wapish wazur na vinywaji utapga hela sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…