Biashara ya vipodozi Vs Electronics

Anza na kile ambacho moyo wako unaamini utaweza kukisimamia na kukufikisha unakotaka.
 
Thanks kwa ushauri mzuri
Biashara ya chakula haijawahi nivutia though najua ina faida kubwa

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru sana kwa ufafanuzi wako makini na wenye kueleweka

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Fungua vipodozi ila usiweke mtaji wote kwanza kwenye mzigo wa kwanza, Anza na mzigo kidogo baada ya hapo ukiona kinachoenda ndio unaagiza zaidi na usiweke frem ikakaa kishua Sana watu wataogopa kuja kununua watajua vitu ni bei ghali. Tafuta uelewa kuhusu aina za vipodozi na ngozi za watu, angalau mteja akija unamshauri ushauri wako ukimsaidia atakuwa mteja wa kudumu. Hiyo Mobile money unaweza kuweka kwenye frem hiyohiyo japo TRA wanaweza kukusumbua leseni
 
Kila biashara lazima kwanza uipende nauwe tayari kuifanya,achana na maswala ya muonekano arif watu tuna sura mbaya shetani anasubiri na tunafanya biashara zakuonana na totoz kila dk na sekunde.

Katika hizo mbili nakushauri pita na vipodozi, kwann vipodozi? vipodozi viko general sana mtu anaweza kuja nunua mafuta tu kashauliza wenzie huko kwako anakuja nunua tu.

anaweza fata sabuni flani,nk nk wateja wengi wa vipodozi wanakuja kununua kitu baada ya wao kufanya research za kitu gani watumie kulingana na ngozi zao au shda wanayokua nayo.

lakini kwenye electronic huku n pautofaut kidogo,una mtaji mdogo sana kwa electronic jambo ambalo litakupa shda kutoka (ila ukikaza unatoka) lakini sijashauri electronic kwasababu huna uelewa wa electronics,wewe si fundi na kwa mtaji huo ili ujaze ujaze duka lazima ujaze maproduct ya kawaida sana hutokua na vitu OG.

sasa Electronic inahitaji ushawishi,kwanini mteja anunue switch hii na sio ile na kwann atumie waya huu na sio ule,electronic haina uongo ukidanganya matokeo kesho yake wanakuletea vitu vimegeuka majivu.

ili upge electronic ungekua na idea na electronic,umepga hata ka cheti kako,unajua zile simple wiring kwamba mteja akipata tatzo unaenda mtatulia mwenyewe vifaa unatoa dukani kwako,ila kwa kusubri mteja aje anunue kitu dukani asee utasubiri.

Electronic kwa mtaji huo hapana labda uchanganye biashara hapo usije ita watu wachawi au ukasema wamekuloga.

wekeza nguvu akili na maarifa kwenye vipodozi,Utatusua.
 
uza vipodozi uniajiri mimi nivutie wateja🤣🤣... am jokin
Uhb ata haumati
 
Mkuu tupe mreJesho.. Ulikuja kuanzisha biashara gan? Na inaendleleaJe?
 
Asante kwa kuuliza. Kimsingi, uamuzi wa biashara ni juu yako kulingana na uwezo wako wa kifedha, ujuzi wako, na matakwa yako binafsi. Hata hivyo, nitajaribu kukupa maoni yangu kulingana na taarifa ulizotoa.

Kwa kuanzia, ningependekeza uanze na biashara ya vipodozi. Biashara hii inahitaji mtaji mdogo sana, na unaweza kuanza na bidhaa chache na kuziweka kwenye duka ndogo au sehemu ya kuuza kwenye barabara. Unaweza pia kuuza bidhaa zako kupitia mtandao kama vile Instagram na WhatsApp.

Pia, biashara ya vipodozi ina wateja wengi sana, hasa wanawake, na unaweza kuongeza mapato yako kwa kuuza bidhaa kwa jumla kwa wauzaji wengine au kwa kuendesha huduma za saluni au kliniki ya urembo.

Kuhusu hofu yako juu ya muonekano, naweza kukuhakikishia kuwa muonekano wa mwenyeji wa duka la vipodozi hauhitajiki sana. Kile kinachohitajika ni bidhaa bora na huduma nzuri kwa wateja wako. Unaweza kujifunza jinsi ya kuwasiliana na wateja vizuri na kuwapa ushauri wa bidhaa wanayohitaji. Pia, unaweza kuajiri mfanyakazi wa kuuza bidhaa kama utahitaji.

Kwa upande wa biashara ya vifaa vya umeme, inahitaji mtaji mkubwa zaidi kuliko biashara ya vipodozi, na pia ina ushindani mkubwa sana. Unaweza kufanya vizuri katika biashara hii ikiwa utakuwa na ujuzi wa kutosha katika uhandisi wa umeme na utaweza kutoa huduma bora kwa wateja wako. Pia, unaweza kuanza na bidhaa chache na kuziongeza kadri biashara yako inavyokua.

Kuhusu wazo la kuweka huduma za mobile money, ni wazo nzuri na inaweza kuongeza mapato yako. Unaweza kuzingatia kuwezekano wa kuweka huduma hii katika biashara yako ya vipodozi, kwani huduma hii inaweza kuwa na mahitaji zaidi kwa wateja wako.

Kwa ujumla, naweza kukushauri uanze na biashara ya vipodozi kama unavyopanga, kwani inahitaji mtaji mdogo na ina wateja wengi, lakini unaweza pia kuchunguza biashara zingine na kuchagua ile ambayo inalingana zaidi na uwezo wako na matakwa yako. Kumbuka kwamba biashara inahitaji uvumilivu, kujituma na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali. Pia, unapaswa kufuata sheria na kanuni za biashara ili kuepuka matatizo na kufanikiwa katika biashara yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…